Tuesday, 13 November 2012

UTPC YATOA VIFAA KWA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA.

Na Derick Milton Mwanza.

Umoja wa vyama vya waandishi wa habari Tanzania [UTPC] umetoa vifaa kwa Klabu za waandishi wa habari 23 tanzania nzima lengo likiwa kuendeleza waandishi wa habari pamoja na kuweza kujitegemea.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa UTPC Abubakar Karsan katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo kwa viongozi wa vyama vya waandishi wa habari mikoa ya Mwanza, Kagera pamoja na Mara waliowakirisha vyama vigine Tanzania nzima.

Alisema  UTPC Kwa kushirikiana na SIDA wametoa dazeni 13 za vifaa kwa kila chama cha waandishi Tanzania nzima, vikiwa vimegarimu kiasi cha shilingi Milioni 800 huku kila chama kikipata vifaa vyenye dhamani ya shilingi Milioni 35.

Alisema kuwa Umoja huo unatoa vifaa hivyo kama wajibu wake katika kuhudumia waandishi wa habari kupitia Klabu zao  Tanzania nzima kwa kutoa misaada ya vifaa vya kutumia katika kazi za kila siku za waandishi wa habari.

Vifaa hivyo ni pamoja na Desktop computer[1],Printer[1],Laptop Computer[1], Ups[1], Binding Machine[1], Lamination Machine[1], Photocopy Machine[1], Multimedia Projector[1], Collapsible Screen[1], Professional Still Picture Camera[1], Digital Tape Recorder[1], DVD Player[1] pamoja na TV Set[1].

Akikabidhi vifaa hivyo kwa viongozi wa Klabu za  waandishi wa habari  wa mikoa iliyowakilisha Klabu zote  Tanzania Rais wa UTPC Kenneth Simbaya alisema umoja umefanya jambo la maana katika kuhakikisha klabu za waandishi wa habari zinajitegemea pamoja na kujiendesha zenyewe.

Aliwataka viongozi wa vyama hivyo kuwajibika katika suala zima la kutunza vifaa hivyo huku akiwataka kuwa wabunifu katika kuvitumia vifaa hivyo,  ili kuleta maendeleo ndani ya chama na kwa waandishi kwa ujumla.

“Kuna Klabu nyingine tulizipa vifaa katika kipindi cha nyuma lakini hadi sasa uwezi ukajua vifaa vile vilienda wapi, hii ni kutokana na viongozi wanaochagulika katika Klabu hizo  kutokuwa makini katika ktunza vifaa vya ofisi wanavyotoa”Alisema Simbaya.

Alisema vifaa hivyo vitaweza kumbadilisha mwandishi kunyanyaswa pindi anapotaka kufanya kazi kazi yake lakini pia vitamfanya mwandishi kuwa huru kwa wakati wote anaotaka kufanya kazi yake.

Aliwaonya waandishi wasio waadilifu kuwa ni chanzo cha kuporomoka kwa maadili ya uandishi wa habari ,huku akiwataka kuwa mfano wa kuigwa katika jamii tunayoihudumia.

No comments:

Post a Comment