Na ALBERT G. SENGO MWANZA
MWENYEKITI wa Chama cha Mpira wa miguu Mkoa wa Mwanza(MZFA) Jackson Songora ametetea nafasi yake kwa miaka mingine minne baada ya kuchaguliwa tena na wajumbe wapatao 17 kati ya 30 wa mkutano mkuu wa chama hicho Mkoani humo.
Uchanguzi huo umefanyika jana katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza ambapo awali wagombea mbalimbali walijinadi kwa wajumbe wa mkutano huo ili kuwashawishi kuweza kuwachagua katika nafasi walizomba ikiwemo ile ya Mwenyekiti, Makamu mwenyekiti, Katibu, Katibu msaidizi, Mweka Hazina na Mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF, Mjumbe mwakilishi wa Vilabu na Mjumbe wa kamati ya udendaji.
No comments:
Post a Comment