Kampeni ya 'Wazazi Nipendeni' licha ya kutumia vyombo mbalimbali vya habari katika kufikisha ujumbe kama vile Radio, Televisheni, Magazeti, Mabango makubwa, Machapisho na mitandao katika kufikisha elimu ya uzazi wa mpango wa mtu binafsi ambao mama wajawazito na wenzi wao wanaoweza kutumia kujiandaa kwa ajili ya kujifungua kampeni hiyo sasa imekuja na mpango wa kufikisha ujumbe kwa njia ya UJUMBE MFUPI WA SIMU yaani SMS.
Mama wajawazito, mama wenye watoto wadogo wa umri wa wiki 16 na wanaowasaidia walituma neno MTOTO kwenda namba 15001 bure bila kulipia ambapo mara baada ya kusajiliwa watatumiwa ujumbe wa maneno bure ambao unahusu mimba salama na huduma za awali kwa mtoto mchanga.
No comments:
Post a Comment