Thursday, 8 November 2012

MAPYA YAIBUKA USHINDI WA RAIS OBAMA BAADA UCHAGUZI.

Baada ya ushindi alioupata Rais Barack Obama wa Marekani  kwa tiketi ya chama chake cha Democratic dhidi ya mpinzani wake  Mitt Romney aliyekua akiwania kiti hicho cha urais kupitia chama cha Republican,kumekuwa na mitizamo tofauti tofauti ya kiimani juu ya ushindi huo wa Rais Obama.
Rais Obama akiwa na familia yake katika shamra shamra za kutoa shukrani kwa wapiga kura kwa kumpa miaka mingine minne kuliongoza taifa hilo la Marekani
Moja ya watu mashuhuri waliojitokeza kuonesha mitizamo yao wakikinzana na ushindi wa rais Obama ni Mchungaji Franklin Graham ambaye pia ni mtoto wa Mhubiri wa kimataifa wa siku nyingi ,Billy Graham wa  Marekani.
Mchungaji Franklin Graham
Akiongea na shirika la Utangazaji la Marekani CNN,  Franklin Graham amesema kwamba, " Taifa la Marekani kwa sasa linaelekea katika njia ya upotevu kutokana na ushindi wa Rais Barack Obama" na hii ikiwa ni kutokana na  msimamo wa Rais Obama kukubaliana na kuhalalishwa kwa ndoa ya jinsia moja ambayo ni kinyume na mpango wa Mungu wa ndoa ya mume mmoja na mke mmoja.
"Kama tunaambiwa kuifuata njia ambayo huyu Rais wetu anataka twende,nadhani itakua ndio kupotea kwetu na uharibifu wa hili Taifa la Marekani @"Rev.Franklin Graham
Kutoka kushoto: ni Mhubiri wa Kimataifa Billy Graham akiwa na mwanae mchungaji Franklin Graham
katika uchaguzi huo  nchini Marekani  kumekuwa na mitizamo tofauti ya kiimani  katika majimbo tofauti tofauti hususan katika suala la ndoa ambapo wanaopinga ndoa ya jinsia moja na kutaka ndoa iwe baina ya Mume mmoja na Mke mmoja  walijikuta wakikabiliwa na upinzani mkali  katika majimbo manne nchini Marekani ambapo  katika majimbo ya Maryland na Washington  walipiga kura wakitetea kuhalalishwa kwa ndoa ya jinsia moja.
wapiga kura katika jimbo la Minnesota wamezuia mabadiliko ya katiba kuingizwa katika katiba ya jimbo hilo hususan suala la ndoa ya jinsia moja huku wapiga kura katika  jimbo jingine la North Star wakipinga vikali ndoa ya jinsia moja.
Rais Barack Obama wakati akitoa speech yake baada ya ushindi wake

majimbo mengine ni pamoja na  jimbo la Maine  ambapo wao wameafiki mabadiliko yanayoruhusu ndoa ya jinsia moja mabadiliko ambayo yalikuwa yakipingwa kwa muda mrefu katika jimbo hilo.

hiki ndicho alichokisema  mchungaji  Franklin Graham.
"God instituted marriage. And for the president to now back something that is against God's position and – is a big problem for him with not only Evangelical churches, but African-American churches across this country who are very conservative," @ Franklin Graham.

baadhi ya matukio yaliyojiri baada ya ushindi wa Rais Obama ni kama inavyoonekana hapa chini
 



No comments:

Post a Comment