TAMKO LA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA MBEYA KUHUSU UCHOCHEZI WA KIDINI
Kwanza kabisa tungependa kutoa pongezi kwa Viongozi na Waumini wa Dini na Madhehebu mbalimbali hapo Mkoa Mbeya kuendeleza utamaduni wetu wa kuishi na kushirikiana katika shughuli mbalimbali za kijamii. Bila kuweka hisia za udini. Tunawashukuru kwa kuendelea kuvumiliana. Pamoja na kuendelea katika hali hii, kumejitokeza viashiria mbalimbali vyenye kuonyesha dalili za kumomonyoka kwa maadili, katika Mkoa wetu.
2. Kumejitokeza baadhi ya viongozi wa dini ambao wamekuwa Wakuzitumia nyumba zetu takatifu za Ibada kuhubiri mambo ambayohayahusiani kabisa na mambo yanayohusu Mwenyezi Mungu na mafundisho yake, kwa kuhubiri mambo ya siasa za chuki kwa dhamira ya kupandikiza chukidhidi ya Serikali au dini na madhehebumengine. Baadhi yao wamediriki kuyasema hayo hadharani kwenye miadhara yao au mikusanyiko ya waumini wao.
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya inaona hali hii haina afya njema kwa mustakabali wa amani na utulivu wa Mkoa wetu na Nchi kwa ujumla. 3. Pamoja na mahubiri hayo pia kumekuwepo nyaraka mbalimbali za kimaandishi za sauti katika kanda, CD zenye kuhubiri chuki, uchochezi dhidi ya dini au dhehebu lingine. Kumekuwepo na video katika kanda, CD au DVD zenye kuhubiri chuki, uchochezi, dharau na kebehi dhidi ya dini nyingine au Serikali na baadhi ya kanda hizo zimediriki kuhamasisha waumini wake vurugu na hata kuua jambo ambalo Kamti ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya inaamini hakuna dini ya aina yoyote dunianiinayohimiza waumini wote kutumia kwa jambo lolote lile. 4. Baada ya kutafakari, Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya imeamua yafuatayo:- inapiga marufuku:
(i) Kuuza, kusambaza au kuonyesha, Kanda za sauti CD za sauti, Kanda za Video, CD, DVD, nyaraka na maandiko yoyte yenye uchochezi wa aina yoyote ile au kukashifu dini yeyote katika Mkoa wa Mbeya.
(ii) Chombo chochote cha Habari kilichopo Mkoani Mbeya kiepuke kuandika makala, kunakili au kurusha hewani hotuba, mahubiri au kuonyesha video zenye kuchochea, kudharau, kuhubiri au kukashifu dini yoyote ile
5. Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa inawaasa viongozi wa dini Mbalimbali kutohubiri siasa kwenye majumba ya Ibada kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanakiuka sheria za nchi. Mtawagawa waumini wenu kwa sababu waumini wanaelewa hayo si maagizo ya Mungu, na hayamo kwenye vitabu vitakatifu.
6. Waandishi wa Habari epukeni kushabikia matamko ya Viongozi wa Dini au Siasa yenye kulenga kuleta mgawanyiko katika taifa hili kwa Misingi ya kidini au kisiasa kwa kisingizio cha Uhuru wa Habari, kumbukeni Amani Umoja na Mshikamano wa Mkoa na Taifa utategemea mchango wenu katika kushabikia au kukemea kauli hizo bila kujali zimetolewa na kiongozi gain.
Mwisho, Serikali itamchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayekwenda kinyume na haya, bila kujali itikadi yake, dini yake au wadhifa wake. Wananchi wanaaswa kuzikabidhi nyaraka, kanda CD na DVD kwa ofisi za Serikali ngazi ya Vijiji, kata Wilaya na Mkoa au kituo chochote cha Polisi. Endapo watakabidhi kwa hiyari hawatachukuliwa hatua.
Imetolewa na:
MWENYEKITI KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA-MBEYA |
No comments:
Post a Comment