Monday, 25 February 2013

PAPA BENEDICT 16 AAGA NA KUWABARIKI MAELFU JUMAPILI YA MWISHO KWAKE


Benedict XVI
©AP/Mail
Hatimaye, ile historia ambayo haijakuwepo kwa takriban miaka 600, inatimia Alhamisi hii ambapo Papa Benedict XVI, atakuwa anaachia rasmi kiti cha uongozi wa Kanisa Katoliki.

Kufuatia hilo, makumi elfu ya wafuasi na watu wamejitokeza kumuaga wakati alipobariki watu kwa jumapili ya mwisho kwake kama Papa, kwenye dirisha lake litazamalo uwanja wa St Peter's Square.

Papa Benedict mwenye umri wa miaka 85, mzawa wa Ujerumani, aliuambia umati uliojitokeza (wakiwemo watalii, waumini, na wakazi wa Roma), wanaokadiriwa kufikia idadi ya watu laki moja, ya kwamba Mungu amemuita kwa njia nyingine hivi sasa - akimtaka kujikita zaidi katika maombi an kutafakari.

"Hii haimaanishi kuwa ninalikacha kanisa, la, bali ni muito kwa kuwa Mungu anataka nimtumikie kwa nguvu na kujitolea kulekule ambao nimejaribu kufanya kwa kipindi chote mpaka hivi sasa. Lakini katika namna ambayo inaendana na umri wangu." Papa alisema kwa sauti yenye nguvu, akiuambia umati huo ambao ulijawa na sura za huzuni.
©AP/Mail
Licha ya mvua kubwa kutabiriwa kunyesha mjini Rome, ambayo ilifanya watu kuhofia kujitokeza, hali haikuwa hivyo, kwani wakati kengele zikilia kuashiria kuwa muda umewadia kwa Papa kuzungumza na watu, mawingu yalitoweka na kuacha jua likimulika kwenye anga ya bluu, jambo ambalo Papa alimshukuru Mungu kwayo, akisema "Tunamshukueu Mungu kwa kutupatia Jua" jambo lililoibua nderemo kwenye umati wa watu hao.

©AP/Mail
Pamoja na hayo yote, bendera zilionekana kupepea miongoni mwa watu, huku bendera ya Brazil ikiongoza kwa wingi, na kwa upande mwingine mtu mmoja Mtaliano akionekana kama mwenye kufanya kampeni kwa kushikilia bango lake lenye majina mawili ya makardinali kutoka nchini humo. 

Uongozi wa kanisa katoliki umekuwa ukichukuliwa kuwa kama nguzo mojawapo ya nchi ya Italy, mpaka pale Papa Yohane alipochaguliwa mwaka 1978 kutoka Poland, kabla ya Mjerumani, Papa Benedict kuchukua nafasi hiyo mnamo mwaka 2005.

No comments:

Post a Comment