SERIKALI wilayani Rungwe imesema kuwa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi ambapo kwa kipindi cha miaka saba vifo hivyo vimepungua kutoka 214 kwa mwaka 2005 hadi kufikia vifo tisa kwa mwaka 2012. Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya hiyo ya Rungwe, Chrispin Meela, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Serikali kwa kipindi cha miaka saba ya serikali ya awamu ya nne. Alisema kuwa sekta ya afya wilayani hapo hususani katika kuhakikisha inafanikiwa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa akina mama, idadi ya vifo hivyo vimepungua na kufikia vifo tisa kati ya wazazi 100,000 wanaojifungua hadi mwaka 2012, kutoka vifo 214 kati ya wazazi 100,000 kwa mwaka 2005. “Idadi ya vifo vya wazazi vilipungua kutoka 214 kati ya wazazi 100,000 kwa mwaka 2005 hadi kufikia vifo 9 kati ya wazazi 100,000 hadi mwaka 2012,” alisema na kuongeza. “Na mafanikio haya yote yametokana na jitihada za makusudi za Serikali kwa kuendelea kutoa hamasa kwa kushirikiana na wadu mbalimbali wa Afya” alisema Mkuu huyo wa Wilaya. Aidha, alisema kuwa katika kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wa chini ya umri wa miaka mitano idadi ya akina mama wajawazito waliojifungulia hospitalini na vituo vya afya waliongezeka kutoka 4,432 hadi kufikia 7, 397. Alisema kuwa hali hiyo ya kuongezeka kwa akina wanaojifungulia hospitalini na vituo vya afya inatokana na wazazi hao kupata huduma iliyobora na salama wakati wa kujifungua hivyo wananachi wenywew wamekuwa wakihamasishana wao kwa wao kwenda kujifungulia sehemu iliyosalama zaidi tofauti na hapo awali. Aidha, alisema kuwa katika kuhakikisha sekta ya afya imeimarishwa zaidi hadi kufikia mwaka 2012 kumekuwepo na Hospitali 3 za ambapo kati ya hizo hospitali moja ni ya Serikali na mbili ni za madhehebu ya dini, zahanati 54 na vituo vya afya vitano. Hata hivyo Mkuu huyo licha ya kuwa na hospitali, vituo vya afya na Zahanati kutoa huduma bora lakini bado kuna changamoto zinazoikabili sekta hiyo kama vile upungufu wa madawa na vifaa vingine vya kutolea huduma kwa wagonjwa. |
No comments:
Post a Comment