Thursday, 14 February 2013

MAISHA NI MAGUMU LAKINI KWA HILI NI HATARI SANA NDUGU ZANGU

A1 
Roli la mafuta aina ya Scania lenye namba za  usajili T 731 ADU likiwa limepinduka  nje kidogo ya mji wa Same jana na kuanza kumwaga mafuta huku polisi wakilinda usalama katika eneo hilo la ajali, Roli hilo linasadikiwa lilikuwa limebeba mafuta aina ya Diesel lita zipatazo  45.000, Lakini jambo la kushangaza ni umbumbumbu wa wananchi, Tamaa na pengine kutokana na hali ngumu ya maisha ambapo walionekana wakiwa na madumu ya Plastiki wakinyonya mafuta hayo baada ya kutokea kwa ajali hiyo jambo ambalo ni hatari sana kutokana na matukio kama hayo mara nyingi husababisha milipuko ya moto na mara nyingi  yamesababisha wananchi kupoteza maisha na kujeruhiwa kwa kuungua moto kutokana na milipuko ya hiyo wakati wananchi wakiiba mafuta katika matukio hayo
Hata hivyo katika eneo hilo la ajali jana Polisi waliwahi na kuwazuia wananchi waliokuwa wakinyonya mafuta hayo na kuwakamata wengine waliokutwa na mafuta kwenye madumu yao.
A2 
Askari polisi wakiimarisha ulinzi katika eneo hilo.
A3 
Vijana wakivizia kuiba mafuta baada ya ajali hiyo kutokea jana nje kidogo ya mji wa Same katika barabara Chalinze kwenda Kilimanjaro na Arusha.

A5 
Wazee, Vijana  kwa Wanawake wakiwa wamekaa kando ya Roli hilo halipo pichani wakisubiri angalau kupata mwanya wa kuiba mafuta ya Diesel kwenye Roli lililopata ajali, hata hivyo ulinzi wa polisi ulikuwa mkali.
A6 
Askari Polisi akiwa amemkamata mmoja wa watu waliokuwa wameiba mafuta katika ajali ya Roli la Mafuta iliyotokea jana Nje kidogo ya Mji wa Same.

No comments:

Post a Comment