Wednesday, 27 February 2013

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya, linawashikilia watu 13, wakiwemo askari wawili wa Jeshi la wananchi (JWTZ) na polisi mmoja kwa matukio ya mauaji na unyang'anyi wa kutumia silaha.


Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya  Diwani Athuman amesema watuhumiwa hao wamewagawanya katika makundi mawili, ambapo kundi la kwanza ni la watuhumiwa 9 wakiwemo askari hao wawili wakidaiwa kuhusika na tukio la kuwaua kikatili na kisha kuwazika dereva na utingo wake
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya  Diwani Athuman akiwa na viongozi wenzake wa jeshi hilo la polisi wakati wa kuongea na waandishi wa habari wa Mbeya
Siraha zilizokamatwa na na jeshi hilo la polisi ndizo zilikokuwa zinatumika na majambazi hayo 
Moja ya bastora iliyotengenezwa kienyeji kwa kutumia vipande vya bomba lakini inatumia risasi za kawaida na nihatari sana siraha hii
Hizi ni vifaa vilivyokamatwa katika matukio mbalimbali yaliotokea mkoani hapa kamanda amewaomba wananchi wa mbeya kuja kuvitambua ofisini kwakwe 
Hizi ni siraha na sare za jeshi ambazo walikuwa wanatumia majambazi hao waliokamatwa kwa tuhuma za mauaji
Waandishi wa habari wakimsikiliza kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya
Mfanyabiashara maarufu wa eneo la Mwanjelwa, Gath Mbilinyi (32), anaetuhumiwa kuteka na kuua
Hawa ndiyo wanaotuhumiwa  kuwaua  dereva na utingo wake na kisha kwenda kuwazika porini  
Samahani kwa picha hizi zinasikitisha haya niamabaki ya miili ya tingo na dereva wake waliouwawa na watuhumiwa hapo juu


JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya, linawashikilia watu 13, wakiwemo askari wawili wa Jeshi la wananchi (JWTZ) na polisi mmoja  kwa matukio ya mauaji na unyang'anyi wa kutumia silaha.

Akizungumza na waandishi habari jijini Mbeya Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya  Diwani Athuman amesema watuhumiwa hao wamewagawanya katika makundi mawili, ambapo kundi la kwanza ni la watuhumiwa 9 wakiwemo askari hao wawili wakidaiwa kuhusika na tukio la kuwaua kikatili na kisha kuwazika dereva na utingo wake.

kundi la pili ni la watuhumiwa wanne wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya dereva wa polisi lililotokea Wilayani Chunya mkoani hapa baada ya kufanyika uporaji wa shilingi milioni 2,200,000 katika kituo cha mafuta eneo la Matundasi wilayani chunya.

Akitoa ufafanuzi zaidi Kamanda Diwani amesema, katika tukio la kwanza ni lile lililotokea Februari 2 katika eneo la Mafinga,Mkoani Mbeya, ambapo watuhumiwa wa kundi la kwanza waliwateka dereva na utingo wake, Festo Kyando (45) na Jafari lililotokea na kuwaua kisha kwenda kuwazika porini.

Amesema dereva huyo alikuwa ametoka Jijini Dar es salaam kubeba mzigo wa wafanyabiashara kwa lengo la kuleta mkoani Mbeya, lakini kumbe walikuwa wakiwindwa na walipofika mkoani Iringa walitekwa na kufanyiwa mauaji hayo ya kinyama.

Kamanda Diwani amesema kufuatia tukio hilo jeshi la polisi lilianza uchunguzi mkali na hatimaye kunasa mtandao huo wa watu 9 wakiwemo askari hao wawili wa jeshi la polisi na JWTZ,ambao uchunguzi umebaini kuwa hutoa mavazi ya majeshi hayo na silaha.

Kamanda Diwani amewataja watuhumiwa hao kuwa MT.85393 Samwel Charles  Balumwina(31) wajiriwa wa jeshi la wananchi kikosi 844 kikosi cha Itende Mbeya na G.1901PC Samwel Kigunye (27) askari wa jeshi la polisi Jijini Mbeya.

Wengine ni mfanyabiashara maarufu wa eneo la Mwanjelwa, Gath Mbilinyi (32), Rajabu Mbilinyi(25), Gregory Mtega(25,Francis Sanga(30) pamoja na ndugu ambao ni wafanyabiashara maarufu katika mji wa Makambako mkoani Njombe ambao ni Japhet Ng'ang'ana(24), Claud Ng'ang'ana(36), Hilally Ng'ang'ana(30)

Hata hivyo amesema walifanikiwa kukamata bidhaa hizo katika eneo la Tunduma ambako tayari zilikuwa zimekamatwa na kwamba miongoni mwa watuhumiwa ndiye aliyeuziwa mzigo huo.

Amesema mali zilizookolewa katika matukio hayo kuwa ni Nondo 397 za aina tofauti pamoja na bando 18 za mifuko ya sandarusi(Sulphate) ambavyo vinashikiliwa na jeshi la Polisi Tunduma Wilani Mbozi Mkoani hapa.

Katika tukio la pili ni lile linalohusisha vifo vya watu wawili wilayani Chunya, ambao ni dereva wa polisi na dereva wa gari la majambazi baada ya kutokea kurushiana risasi.
Amesema tukio hilo lilitokea Februari 6 baada ya watuhumiwa wanne ambao wanashikiliwa na jeshi hilo kufanya uporaji wa shilingi milioni 2,200,000 katika kituo cha matundasi wilayani humo.
Amewataja madereva hao waliouwawa katika tukio hilo kuwa ni dereva wa polisi aliyefahamika kwa jina moja la Jafari, ambapo yule wa majambazi akitajwa kwa jina la  Shabani John.
Diwani amewataja watuhumiwa wanashikiliwa kwa tukio hilo kuwa ni Manase Kibona (37).Emmanuel Mndendemi na Masai Hongole, Mashaka George, John Mahenge, Narasco Mabiki.

Kamanda huyo amezitaja mali zilizookolewa katika matukio hayo kuwa ni Nondo 397 za aina tofauti pamoja na bando 18 za mifuko ya sandarusi(Sulphate) ambavyo vinashikiliwa na jeshi la Polisi Tunduma Wilani Momba  Mkoani Mbeya.

Aidha,kamanda Diwani  amevitaja baadhi ya vielelezo vilivyokamatwa  kuwa ni Bunduki aina ya Shot Gun moja ambayo namba zake zilifutika, Gobore moja ambalo pia namba zake zilifutika, Bastora tatu zilizotengenezwa kienyeji zisizo na namba na zinazotumia risasi za s/Gun.

Vingine ni Risasi 31 za Silaha ya SMG/SAR, Sare za Jeshi (JWTZ), suruali 4, mashati 4 kofia 3 na Viatu jozi mbili , Risasi 99 za S/GUN, Risasi 25 za Bastola na magari yenye namba T 464BLX TOYOTA COROLA,T381 BDR VITZ, T 251 AKU Toyota Pick Up ,T 193 BDY  Toyota Premio na T 214 ASV  Toyot Mark II.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi anawashukuru wananchi wa Mkoa wa Mbeya waliojitokeza katika ktoa ushirikiano wa kuwasaka majambazi hayo ambapo pia anaendelea kutoa wito kwa watu wenye taarifa za watu ambao haeajakamatwa.
Ameongeza kuwa taratibu za upelelezi zimekamilika ambapo taratibu za kuwafikisha mahamakamani zinaendelea.
   

WIZI WA MTANDAO KUPITIA ATM

watu wanne washikiriwa na jeshi la polisi wilayani Rungwe mkoani Mbeya kwa tuhuma za kukutwa na ATM card 150 za Benki ya NMB na rist ya majina na namba za siri za kadi hizo usiku wa kuamkia leo na kufanikiwa kuchukua pesa kiasi cha TSH 20,543,200/=

watu wanne washikiriwa na jeshi la polisi wilayani Rungwe mkoani Mbeya kwa tuhuma za kukutwa na ATM card 150 za Benki ya NMB na rist ya majina na namba za siri za kadi hizo usiku wa kuamkia leo na kufanikiwa kuchukua pesa kiasi cha TSH 20,543,200/

Monday, 25 February 2013

ACHA KUSUMBUKA JIUNGE SASA Airtel NI ZAIDI YA BURE


PAPA BENEDICT 16 AAGA NA KUWABARIKI MAELFU JUMAPILI YA MWISHO KWAKE


Benedict XVI
©AP/Mail
Hatimaye, ile historia ambayo haijakuwepo kwa takriban miaka 600, inatimia Alhamisi hii ambapo Papa Benedict XVI, atakuwa anaachia rasmi kiti cha uongozi wa Kanisa Katoliki.

Kufuatia hilo, makumi elfu ya wafuasi na watu wamejitokeza kumuaga wakati alipobariki watu kwa jumapili ya mwisho kwake kama Papa, kwenye dirisha lake litazamalo uwanja wa St Peter's Square.

Papa Benedict mwenye umri wa miaka 85, mzawa wa Ujerumani, aliuambia umati uliojitokeza (wakiwemo watalii, waumini, na wakazi wa Roma), wanaokadiriwa kufikia idadi ya watu laki moja, ya kwamba Mungu amemuita kwa njia nyingine hivi sasa - akimtaka kujikita zaidi katika maombi an kutafakari.

"Hii haimaanishi kuwa ninalikacha kanisa, la, bali ni muito kwa kuwa Mungu anataka nimtumikie kwa nguvu na kujitolea kulekule ambao nimejaribu kufanya kwa kipindi chote mpaka hivi sasa. Lakini katika namna ambayo inaendana na umri wangu." Papa alisema kwa sauti yenye nguvu, akiuambia umati huo ambao ulijawa na sura za huzuni.
©AP/Mail
Licha ya mvua kubwa kutabiriwa kunyesha mjini Rome, ambayo ilifanya watu kuhofia kujitokeza, hali haikuwa hivyo, kwani wakati kengele zikilia kuashiria kuwa muda umewadia kwa Papa kuzungumza na watu, mawingu yalitoweka na kuacha jua likimulika kwenye anga ya bluu, jambo ambalo Papa alimshukuru Mungu kwayo, akisema "Tunamshukueu Mungu kwa kutupatia Jua" jambo lililoibua nderemo kwenye umati wa watu hao.

©AP/Mail
Pamoja na hayo yote, bendera zilionekana kupepea miongoni mwa watu, huku bendera ya Brazil ikiongoza kwa wingi, na kwa upande mwingine mtu mmoja Mtaliano akionekana kama mwenye kufanya kampeni kwa kushikilia bango lake lenye majina mawili ya makardinali kutoka nchini humo. 

Uongozi wa kanisa katoliki umekuwa ukichukuliwa kuwa kama nguzo mojawapo ya nchi ya Italy, mpaka pale Papa Yohane alipochaguliwa mwaka 1978 kutoka Poland, kabla ya Mjerumani, Papa Benedict kuchukua nafasi hiyo mnamo mwaka 2005.

MTOTO AFUFUKA TUMBONI BAADA YA MAOMBI


Mama ambaye Mungu amemtendea muujiza siku ya jana kanisani Kawe!

Mtoto afufuka akiwa ndani ya tumbo, kanisani Ufufuo na Uzima Kawe jana:

Tukio hilo lililowaacha watu waliokuwepo kanisani kwa mshangao na kumshukuru Mungu, ni baada ya mama aliyekuwa mjauzito wa miezi saba kuja kanisani pamoja na karatasi za daktari kuwa mwanaye amefariki akiwa ndani ya tumbo.

Akieleza kwa machungu kabla ya kufufuka kwa mwanaye, mama huyo alisema kuwa, huo ulikuwa ujauzito wa pili baada ya mara ya kwanza mtoto wake kutoka kabla ya muda. "Lakini jambo hilo limejirudia tena kwa mtoto huyu wa pili maana baada ya kwenda hospitali niliambiwa kuwa mtoto wangu amekwisha fariki" alisema mama huyo.

Mchungaji Josephat Gwajima alimuombea, na dakika ile ile mama huyo alisikia mtoto akicheza ndani ya tumbo jambo ambalo lilimwacha mama huyo akiwa na furaha... "Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakao onekena tele wakati wa mateso".

Friday, 22 February 2013

VIONGOZI na Watumishi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano na vyama vya siasa vya upinzani ili kuwaletea maendeleo wananchi.


Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dk. Norman Sigalla ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya wakati akifungua warsha juu ya Demokrasia na Stadi za uongozi inayotolewa kwa viongozi wa Chama cha Mapinduzi pamoja na Madiwani wa Mkoa wa Mbeya.
Mwaandaaji wa Mafunzo hayo Dk. Marry Mwanjelwa Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Mbeya

Mfadhili wa Mafunzo hayo Dk. Stefan Chrobot ambaye ni Mkurugenzi Mkazi wa shirika la Fes- Tanzania kutoka Ujerumani 

Katibu wa CCM wilaya ya Mbeya mjini, Raymond Mwangwala,






VIONGOZI na Watumishi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano na vyama vya siasa vya upinzani ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dk. Norman Sigalla ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya wakati akifungua warsha juu ya Demokrasia na Stadi za uongozi inayotolewa kwa viongozi wa Chama cha Mapinduzi pamoja na Madiwani wa Mkoa wa Mbeya.
  
Dk. Sigalla alisema Chama cha Mapinduzi ni mlango wa kuingilia ili kupata uongozi ili kuwahudumia wananchi lakini siyo sababu ya kuwachukia viongozi wa vyama vya upinzani.
  
" Si sahihi kugombana na na kiongozi wa chama kingine bali shirikianeni ili muwaletee maendeleo wananchi ambapo mtakapokuwa na ushirikiano na upendo ndipo watakapo watamani na kuhamia kwenye chama chenu" alisema Mkuu huyo.
  
Aliongeza kuwa Warsha zinazotolewa kwa viongozi zinasaidia kuwakumbusha wajibu wao kwa chama na kwa wananchi ili wasijisahau katika utendaji kazi wa kila siku ikiwa ni pamoja na kutekeleza Ilani za Chama.
Alisema kazi ya kiongozi wa Chama ni kujibu hoja za wananchi na siyo kiongozi kujifanyia mambo ambayo wananchi hawayahitaji na ambayo yanasababisha kuwachukia viongozi.
  
Kaimu Mkuu wa Mkoa huyo alisema ili Chama kiendelee kubaki madarakani ni wajibu wa Viongozi waliopewa dhamana na wananchi kuyatendea kazi madai yao ambayo yataepusha migogoro isiyokuwa na sababu.
  
Kwa upande wake Mwaandaaji wa Mafunzo hayo Dk. Marry Mwanjelwa Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Mbeya alisema mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya mkutano mkuu wa wajumbe wa CCM Taifa walioagizwa kuwajengea uwezoviongozi wa Chama.
  
Alisema lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuwakumbusha viongozi waliokuwepo madarakani kuhusu uwajibikaji pamoja na kuwajengea uwezo viongozi wapya walioingia madarakani hivi karibuni.
  
Naye mfadhili wa Mafunzo hayo Dk. Stefan Chrobot ambaye ni Mkurugenzi Mkazi wa shirika la Fes- Tanzania kutoka Ujerumani alisema wameamua kufadhili mafunzo hayo kutokana na shirika hilo kuwa na ushirikiano na Chama cha Mapinduzi.
  
Alisema kazi ya Shirika hilo ni kukuza demokrasia na utawala katika jamii, kuinua haki za binadamu za kupata huduma muhimu za kijamii na namna ya kuepukana na rushwa.

TAMKO LA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA MBEYA KUHUSU UCHOCHEZI WA KIDINI


MWENYEKITI
KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA-MBEYA
NORMAN SIGALLA 


BAADHI YA VIONGOZI WA
KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA-MBEYA

MWANDISHI WA HABARI FELIX MWAKYEMBE AKIULIZA SWALI KWA KAMATI HIYO
EMMANUEL LENGWA  MWANDISHI  AKIULIZA SWALI KWA KAMATI HIYO YA ULINZI YA MKOA WA MBEYA
MOJA YA WANAKAMATI YA ULINZI MKOA WA MBEYA KAMADA DIWANI AKIJIBU BAADHI YA MASWALI YALIOULIZWA NA WAANDISHI WA HABARI 

TAMKO LA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA MBEYA KUHUSU UCHOCHEZI  WA KIDINI

Kwanza kabisa tungependa kutoa pongezi kwa Viongozi na Waumini wa Dini na Madhehebu mbalimbali hapo Mkoa Mbeya kuendeleza utamaduni wetu wa kuishi na kushirikiana katika shughuli mbalimbali za kijamii. Bila kuweka hisia za udini. Tunawashukuru kwa kuendelea kuvumiliana. Pamoja na kuendelea katika hali hii, kumejitokeza viashiria mbalimbali vyenye kuonyesha dalili za kumomonyoka kwa maadili, katika Mkoa wetu.

    2.   Kumejitokeza baadhi ya viongozi wa dini ambao wamekuwa   
Wakuzitumia nyumba zetu takatifu za Ibada kuhubiri mambo  ambayohayahusiani kabisa na mambo yanayohusu Mwenyezi Mungu na mafundisho yake, kwa kuhubiri mambo ya siasa za chuki kwa dhamira ya kupandikiza chukidhidi ya Serikali au dini na madhehebumengine. Baadhi yao wamediriki kuyasema hayo hadharani kwenye miadhara yao au mikusanyiko ya waumini wao.


   Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya inaona hali hii haina  
   afya njema kwa mustakabali wa amani na utulivu wa Mkoa wetu na    
   Nchi kwa ujumla.
3.               Pamoja na mahubiri hayo pia kumekuwepo nyaraka mbalimbali za kimaandishi za sauti katika kanda, CD zenye kuhubiri chuki, uchochezi dhidi ya dini au dhehebu lingine. Kumekuwepo na video katika kanda, CD au DVD zenye kuhubiri chuki, uchochezi, dharau na kebehi dhidi ya dini nyingine au Serikali na baadhi ya kanda hizo zimediriki kuhamasisha waumini wake vurugu na hata kuua jambo ambalo Kamti ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya inaamini hakuna dini ya aina yoyote dunianiinayohimiza waumini wote kutumia kwa jambo lolote lile.
4.               Baada ya kutafakari, Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa  Mbeya imeamua yafuatayo:- inapiga marufuku:

(i)               Kuuza, kusambaza au kuonyesha, Kanda za sauti CD za sauti, Kanda   
za Video, CD, DVD, nyaraka na maandiko yoyte yenye uchochezi wa aina yoyote ile au kukashifu dini yeyote katika Mkoa wa Mbeya.

(ii)             Chombo chochote cha Habari kilichopo Mkoani Mbeya kiepuke   
           kuandika makala, kunakili au kurusha hewani hotuba, mahubiri au   
           kuonyesha video zenye kuchochea, kudharau, kuhubiri au kukashifu 
           dini yoyote ile 


  
5.       Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa inawaasa viongozi wa dini
 Mbalimbali kutohubiri siasa kwenye majumba ya Ibada kwani kwa   
 kufanya hivyo watakuwa wanakiuka sheria za nchi. Mtawagawa       
 waumini wenu kwa sababu waumini wanaelewa hayo si maagizo ya 
 Mungu, na hayamo kwenye vitabu vitakatifu.


6.       Waandishi wa Habari epukeni kushabikia matamko ya Viongozi wa   
          Dini au Siasa yenye kulenga kuleta mgawanyiko katika taifa hili kwa  
          Misingi ya kidini au kisiasa kwa kisingizio cha Uhuru wa Habari,  
          kumbukeni Amani Umoja na Mshikamano wa Mkoa na Taifa
          utategemea mchango wenu katika kushabikia au kukemea kauli hizo
          bila kujali zimetolewa na kiongozi gain.


Mwisho, Serikali itamchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayekwenda kinyume na haya, bila kujali itikadi yake, dini yake au wadhifa wake. Wananchi wanaaswa kuzikabidhi nyaraka, kanda CD na DVD kwa ofisi za Serikali ngazi ya Vijiji, kata Wilaya na Mkoa au kituo chochote cha Polisi. Endapo watakabidhi kwa hiyari hawatachukuliwa hatua.

Imetolewa na:

MWENYEKITI
KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA-MBEYA

Wednesday, 20 February 2013

USIKOSE KATIKA MKUTANO MKUBWA WA INJIRI KATIKA UWANJA WA SAMORA


MKUTANO MKUBWA WA INJIRI IRINGA KUUNGURUMA KATIKA UWANJA WA SAMORA KUVUNJA NGUVU ZA KICHAWI.

Hizi ni siku kumi za miujiza mikubwa ambayo haijapatakutokea katika mkoa wa Iringa kuanzia terehe 23/03/2013 hadi tarehe 03/03/2013, ni katika mkutano mkubwa wa kuvunja na kuharibu nguvu za kichawi ambazo zimekuwa zikiwatesa watu kwa muda mrefu sasa zinakenda kukomeshwa ambapo maandalizi ya mkutano huo yamekamilika na Wahubiri wa kimataifa zaidi ya wanne watakuwepo kuwahudumia watu wa mikoa ya nyanda za juu kusini,ikiwa ni pamoja na mwenyeji wa mkutano Askofu Boaz Sollo, Mtume Ken Gitonga,Bonefasi Indeche pamoja na Dastan Maboya ambapo Askofu Dk.Boaz Sollo alithibitisha kwamba huu ni mkutano ambao haujawahi kufanyika iringa na aliwataka wakazi wa Iringa kushiriki kikamilifu katika mkutano huo ili waweze kuziona Baraka za Mungu katika maisha yao.
   
Wakati huohuo wakristo nchi wametakiwa kumtumaini mungu na siyo kuogopa nguvu za Kishirikina. 
Hayo yamesemwa na askofu wa huduma ya overcomers power centre pamoja na makanisa ya End Time And Havesting Church Dr.Boaz Sollo alipokuwa akifundisha katika ibada zilizofanyika mfululizo wiki iliyopita ikiwa ni moja ya masomo yanayoendelea kufundishwa na mtumishi huyo na kuwataka waumini wa kanisa hilo kutambua namna wanavyo weza kuzishinda nguvu za kichawi ambazo mara nyingi zimeonekana kuwasumbua watu wengi hususani katika mkoa wa Iringa.

Askofu Boaz aliwataka wazazi kutambua umuhim wa kuwalinda watoto wao kwa maombi ili kuwakinga watoto hao na nguvu za kichawi ambazo pia zimeendelea kuwatesa watoto huku wengine wakittumikishwa na kushughulishwa na shughuli za kishirikina lakini pia wengi wameshindwa kuendelelea na masomo kutokana na nguvu za kishirikina,hivyo a matendo ya mitume 13.6 akazungumzia habari za watu kama Bayesu au Elima aliyekuwa akimuhudumia liwali aliyekuja kuokoka na elima kufanya mbinu za kumfanya aache imani kwa hilo pia unaweza kuona jinsi wachawi wanavyofanyakazi ya kurudisha nyuma imani za watu waliomjua mungu kutokana na shuhuda mbalimbali ambazo watu wameweza kushudia na Mungu amejidhihirisha wazi kwamba kuna jambo ambalo mungu ametenda kwa watu wa Iringa kupiia huduma ya mtumishi wa Mungu Askofu Boaz solo,ikiwa bado somo hilo linalo husiana katika mkutano wa Samora Iringa.

MHESHIMIWA DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA AMETOA ZAIDI YA TANI MOJA YA MIFUKO YA SARUJI NA KUHAMASISISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI KATA YA ITAGANO JIJINI MBEYA



DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA AKIWEKA TOFARI KUHAMASISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI ITAGANO 
HAPA MWESHIMIWA DR. MARYA MWANJELWA AKIENDELEA NA UJENZI WA KUPANDISHA UKUTA WA DARASA MOJA

DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA  AKIMKABIDHI MIFUKO YA SARUJI ZAIDI YA TANI MOJA MWESHIMIWA DIWANI KATA YA ITAGANO MBWIGA NDALAMA KWA AJILI YA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI ITAGANO
NAE MWESHIMIWA DIWANI WA KATA YA ITAGANO MBWIGA NDALAMA AKIMSHUKURU MWESHIMIWA MBUNGE DR.MARY MWANJELWA KWA KUTOA MSAADA HUO NA PIA KUWAHAMASISHA KATIKA UJENZI WA SHULE HIYO YA SEKONDARI ITAGANO DIWANI HUYO AMESEMA KUWA SHULE HIYO ITAKAPOKAMILIKA ITASAIDIA HATA WATOTO WA VIJIJI JIRANI NA KATA HIYO KUAPATA ELIMU YA SEKONDARI  PIA WAMEMWAHIDI MWESHIMIWA MBUGE KUWA MADARASA MATATU MPAKA KUFIKIA MWEZI WA SITA YATAKUWA YAMEKAMILIKA NA TAYARI KWA KUTUMIWA
HAPA MWESHIMIWA MBUNGE AKIPATA MAELEZO TOKA KWA MWESHIMIWA DIWANI WA KATA YA ITAGANO JINSI UJENZI WA MADARASA HAYO UTAKAVYOKAMILIKA MAPEMA MARA BAADA YA KUKABIDHIWA SARUJI
MWESHIMIWA MBUNGE AKIONGEA NA WAKAZI WA KATA YA ITAGANO MARA BAADA YA KUKABIDI MSAADA HUO WA MIFUKO YA SARUJI
HII NDIYO SHULE YA SEKONDARI ITAGANO AMBAYO MWESHIMIWA DR MARY MWANJELWA AMETOA MSAADA  WA MIFUKO YA SARUJI
MARA TU BAADA YA KUMALIZA UTOAJI WA MSAADA PAMOJA NA UHAMASISHAJI WA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI ITAGANO MWESHIMIWA MBUNGE ALIPATA NAFASI YA KUONGEA NA KINA MAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI KATA YA ITAGANO

SERIKALI YA MBOZI YAKABIDHI MAABARA ZINAZOHAMISHIKA NNE KWA SHULE ZA SEKONDARI


 MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA MBOZI LEVISON CHILLEWA AKIMKABIDHI DIWANI WA MSIA MH MAKUNGANYA MOJA YA MEZA ZILIZOTOLEWA KUFUATIA MSAADA WASERIKALI WA KIASI CHA SHILINGI MILION 24 KWA HALMASHAURI ZOTE NCHINI KWAAJILI YA KUBORESHA MAABARA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI 
 MMOJA WA WATAALAMU WA MAABARA AKIONYESHA NAMNA ZANA HIZO ZINAVYOFANYA KAZI KABLA YA KUKABIDHIWA KWA WAKUU WA SHULE ZA KATA WALIOONGOZANA NA MADIWANI WAO
 MIONGONI MWA SHULE ZA KATA ZENYE UHITAJI WA VIFAA NA MAABARA AMBAPO KWA MIAKA TAKRIBANI SITA WATOTO WAMEKUWA WAKISOMA BILA KUFANYA MAZOEZI YA VITENDO 
 AFISA ELIMU SEKONDARI WILAYA YA MBOZI BWANA ISAACK MGAYA AKIPEWA MKONO WA SHUKRANI NA BAADHI YA WALIMU NA DIWANI WA KATA YA RUANDA BAADA YA SHULE YA LUMBILA KUPEWA MEZA YA MAABARA INAYPOTEMBEA
 MIONGONI  MWA ZANA ZITAKAZOGAWIWA MASHULENI KWAAJILI YA KUIMARISHA MAFUNZO KWA VITENDO
OFISA KATIKA IDARA YA ELIMU SEKONDARI AKIONYESHA NAMNA YA KUUNGANISHA  MFUMO WA MAJI KWENYE MEZA YA MAABARA


HALMASHAURI ya wilaya Mbozi imekabidhi meza nne za maabara inayotembea kwaajili ya mafunzo ya vitendo katika masomo ya Baiolojia, Kemia , Kilimo na Fizikia kwa shule nne za sekondari ikiwa ni sehemu ya hatua za kukabili changamoto za matokeo mabaya ya shule za sekondari katika masomo ya sayansi.
Afisa Elimu sekondari wilayani Mbozi bwana Isaack Mgaya, amesema meza hizo zenye thamani ya shilingi Milion 24 zinatokana na msaada uliotolewa na serikali mwezi juni wa kiasi hicho cha fedha kwaajili ya kuziwezesha shule za sekondari kuwa na Maabara zinazohamishika.
Amesema hatua hiyo inaziwezesha shule Mbili za sekondari kwa wilaya mpya ya Momba za Mkulwe na Nkangamo kuwa na maabara wakati kwa upande wa wilaya ya Mbozi shule za sekondari za Msia na Lumbila pia zimenufaika.
Bwana Mgaya amesema Mobile Laboratory kama zinavyofahamika zimebuniwa ili kuwezesha kukidhi mafunzo ya masomo ya sayansi kwa vitendo katika shule za sekondari na Vyuo.
Aidha alifafanua kuwa matumizi yake yanawezesha madarasa hayo kuhama hama kulingana na mahitaji na kwamba pia zinaweza kutumika chini ya miti, ama maeneo yasiyo na mifumo ya umeme ama maji hivyo kurahisisha uelewa wa wanafunzi kulingana na mazingira waliyopo
kwa upande wake mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Wilaya ya Mbozi bwana Levison Chilewa ambaye aliambatana na Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Momba Bwana Juma Kitabuge ameeleza kuwa kutokana na muundo wa maabara hizo, madiwani wa kata zilizonufaika na mpango huo wanapaswa kujenga hoja za kushawishi madiwani wenzao ili kutenga kiwango kikubwa cha fedha za mapato ya ndani ya halmashauri hizo mbili kwaajili ya ununuzi wa meza hizo ambazo zitakuwa mkombozi kwa watoto katika masomo ya sayansi.
Alisema hivi sasa wanafunzi wamekuwa waoga wa masomo hayo kutokana na mazingira ya kusomea kutokuwa yenye mvuto ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa zana muhimu na maabara, na kwamba hatua ya kusambazwa kwa teknolojia hiyo rahisi kunawawezesha wanafunzi sasa kujifunza katika hali iliyobora zaidi kwa vitendo.
Alisema ni vyema pia kwa shule zilizo karibu kuona namna ambavyo zinaweza kushirikiana kutumia maabara moja kwa kutembeleana hatua ambayo itarahisisha katika ufundishaji na hata kuleta tija katika matumizi ya maktaba hizo badala ya kuazimisha meza hizo kutoka shule moja kwenda shule nyingine hali ambayo inaweza kusababisha uharibifu.
Akizungumzia msaada huo, diwani wa kata ya Ruanda bwana Keneth Mgala amesema, kimsingi hatua hiyo itasaidia kupunguza hali ya matokeo mabaya kwenye masomo ya sayansi ambapo wanafunzi wakti mwingine wanalaumiwa kwa kuonewa kutokana na mazingira yenyewe ya shule kukosa vitu muhimu kama maabara hivyo kushindwa kuhamisha nadharia katika vitendo ama kuoanisha vyote viwili.
Kwa kipindi kirefu,Shule pekee yenye maabara ya kubuniwa na utundu wa mwalimu mmoja wilaya ya Mbozi ipo katika shule ya sekondari ya Vwawa ambapo maaabara hiyo imekuwa  shule kadhaa zimekuwa zikitembelea na  kujifunza ubunifu huo kwa lengo la kwenda kutengeneza katika shule zingine ili kuongeza hamasa ya  wanafunzi kupenda masomo ya sayansi