![]() |
Baptist Chipikizi Kwaya |
Moja kati ya kwaya zinazofanya vizuri katika anga la muziki wa injili Mwanza na Kanda ya Ziwa Baptist Chipukizi Choir kutoka Usagara Mwanza wametibithisha kushiriki katika Pasaka Gospel Festival 2013 katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Wakiongea na mtandao huu wamesema wao wamejipanga vizuri kuja kutimiza kusudi la kusherehekea pasaka kwa kishindo kisichokuwa cha kawaida kama jinsi watu wanavyowajua.
Pasaka Gospel Festival 2013 inayoandaliwa na Cosu Entertainment itafanyika jumapili 31/3/2013 katika uwanja wa CCM Kirumba na 1/4/2013 katika uwanja wa CCM Katoro Geita.
Huku wakazi wa mikoa wa Mwanza, Geita, Mara, Kagera, Shinyanga, Simiyu, Kigoma na Tabora wakiwa na ari ya kushuhudia Pasaka Gospel Festival kwa uhalisia wake.
Pasaka Gospel Festival 2013 litaongozwa na Mkali wa Muziki wa Injili kutoka Dar es salaam Enock Jonas Zunguka Zunguka, na Gwiji wa muziki afrika masahariki Neema Mwaipopo na wasanii wengine kumi kutoka Dar, Mbeya, Arusha, Tabora, na Iringa.
Kwaya zaidi ya kumi na tano zitapiga kambi kwa ajili ya kutumbuiza katika tamasha hilo kwa kingilio cha 2000/= kwa wote.
No comments:
Post a Comment