Wednesday, 13 March 2013

PASAKA GOSPEL FESTIVAL 2013 CCM KIRUMBA MWANZA PASAKA GOSPEL FESTIVAL 2013 CCM KIRUMBA MWANZA, KUTANA NA ISAYA MSANGI KATIKA WIMBO WAKE SHETANI IMEKULA KWAKO. USIKOSE SIKU HIYO. Isaya Msangi - Shetani Imekula Kwako


Mwimbaji wa anayetisha katika Muziki wa Injili kutoka Dar es salaam Isaya Msangi anayetamba na wimbo wake wa shetani imekula kwako amesema anakuja Mwanza kwenye Pasaka Gospel Festival kuwapa Raha wakazi wote wa Jiji la Mwanza na Mkoa wa Geita.

Msangi ambaye amezindua albamu yake Jumapili iliyopita Jijini Dar es salaam amesema kuwa kutokana na kukubalika sana mikoa hasa Mwanza amewaomba watu wote wajitokeze kujionea jinsi Mungu anavyomtumia katika nyimbo za Injili.

 Mbali na Isaya Msangi, katika Tamasha Hilo La Pasaka Gospel Festival 2013 wapo waimbaji kama Enock Jonas,Neema Mwaipopo, Nesta Sanga, Daniel Safari, Jessica Julius, John Shaban wote kutoka Dar es salam, Kutoka Mbeya yupo Tumaini Mbembela, Kutoka Iringa Dan Sanga na Arusha yupo Neema Munis. Pia wapo waimbaji na kwaya kali kutoka Mkoa wa Mwanza na Geita katika kusherekea sikukuu ya Pasaka.

Pasaka Gospel Festival 2013 litafanyika tarehe 31/3/2013 katika uwanja wa ccm kirumba na tarehe 1/4/2013 katika uwanja wa ccm katoro Geita kwa kiingilio cha 2000/= kwa kila mtu.

Karibuni sana watanzania wote wa dini, rangi, rika zote.

No comments:

Post a Comment