Thursday, 14 March 2013

ENOCK JONAS ZUNGUKA ZUNGUKA NDANI YA JIJI LA MWANZA NA GEITA PASAKA GOSPEL FESTIVAL 2013

Mwimbaji anayetisha sana katika medani ya muziki wa injili ENOCK JONAS ambe anatamba na wimbo wake wa Zunguka Zunguka, amesema Pasaka ya Mwaka huu atakula na wakazi wa jiji la Mwanza na Geita na hii ni kutokana na mapenzi aliyonayo kwao.

Enock Jonas amesema anakuja kutambulisha albaumu yake mpya iitwayo NIPE MDUNDO albamu ambayo ina kila sababu ya kupewa sapoti na wadau wote wa muziki wa Injili kanda ya ziwa.

Pasaka Gospel Festival 2013 litafanyika tarehe jumapili tarehe 31/3/2013 katika uwanja wa CCM Kirumba na tr 1/4/2013 katika uwanja wa CCM Katoro Geita kwa kiingilio 2000/= kwa kila mtu.

No comments:

Post a Comment