Miongoni mwa kauli nzuri zilizotolewa na Askofu wa kanisa hilo Dk Boaz Sollo alisema miongoni mwa malengo ya ujenzi wa kanisa hilo ni kuhakikisha watu wa mkoa wa Iringa na nchi nzima wanabadilishwa mitazamo ya kidunia na kuachana na kumgeukia mungu lakini pia ni kuwa kanisa litakalohakikisha watu wa mkoa wa Iringa wana pata mafundisho ili kujikwamua kiuchumi kiroho na pi ni kutengeneza mahusiano mazuri ya kiroho na waumini wa madhebu mengine hasa kupitia kituo cha Redio ya Kanisa hilo iitwayo OVERCOMERS FM ambayo ni maarufu katika mikoa ya nyanda za juu kusini inayopatikana katika masafa ya 98.6 Iringa.
Huduma inayotolewa na kanisa la Overcomers Power Centre imefanyika Baraka kubwa kwa wakazi wa mikoa hiyo ya nyanda za juu kusini na Tanzania kwa ujumla na hii inajidhihirisha kutokana na jinsi watu wanavyofunguliwa pia wanavyo barikiwa na kufanikiwa katika maisha yao.
Harambee ya uchangiaji fedha kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa kanisa hilo.
Ili kuthamini michango inayotolewa na viongozi mbalimbali hapa nchini katika kuhakikisha kazi ya mungu inasonga mbele Kanisa la Overcomers Power Centre Iringa chini ya mtumishi wa Mungu Askofu Dk Boaz Sollo limeandaa tuzo maalum nayaheshima kwaajili ya kumtunuku Waziri mkuu aliyejihuzuru Mh Edwadi Lowasa ambaye ndiye atakayekuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo inayotarajiwa kufanyika tarehe 21/04/2013 hapo mkoani Iringa kwaajili ya ujenzi huo.
Akizungumzia kuhusu tuzo hiyo Askofu wa kanisa hilo Dk Boaz Sollo amesema kwa kutambua mchango wa kiongozi huyo wa nchi katika kuyasaidia makanisa pamoja na shughuli za kijamii wameona ni vyema kumtunuku tuzo ya Heshima ili kumtia moyo kwa kazi anayo ifanya kwa jamii pamoja na changamoto nyingi anazokutana nazo wakati wa kujitolea na kusaidia suala la maendeleo katika jamii hasa wale wanao mpinga katika hilo ili kumkatisha tamaa hivyo Askofu Boaz Sollo pamoja na waumini wa kanisa hilo wataendelea kumuombea ili afanikiwe zaidi pamoja na kushinda vikwazo vinavyomkabili kiongozi huyo.
"tunatambua mchango wake kwa jamii na amesaidia makanisa mengi wau wengi pamoja na vikundi vingi kwakweli ni mtu wa watu kwa kuliona hilo tumeona siku hiyo ya Harambee tutamtunuku Tuzo ya heshima ili kumtia moyo na asikate tamaa kuendelea kuwasaidia watu mbalimbali pale wanapomuhitaji"
"tumeona mchango wake na tumeguswa na hilo sisi tutendelea kumuombe kwa Mungu ili afanikiwe katika yale anayoyafanya hata kama kuna watu wanaompinga hii inatokana kwamba siku zote tunaamini shetani hapendi maendeleo ya mtu wa Mungu"alisema askofu.
Kwa upande wa wananchi wa mkoa wa Iringa walipongeza kanisa hilo kwa kukumbuka kumpa tuzo kiongozi hiyo ambaye tangu ajihuzuru uongozi wake hakuwahi kufika Iringa na ameendelea kujitolea katika shughuli za jamii bila kubagua rangi au kabila la watu anaoweza kuwasaidia,hivyo wanamsubiri kwa hamu kubwa ili kumuunga mkono kwa shughuli atakayo ifanya ya kuongoza uchangiaji wa ujenzi wa nyumba ya bwana
Haya ni majengo ya Ofisi pamoja na kituo cha redio ya Overcomers fm
![]() |
Jengo hili la Ofisi za kanisa hilo pamoja na Kituo cha Redio |
![]() |
Mafundi wakiendelea na kazi ya Ujenzi wa ofisi za kanisa |
![]() |
Upende wa nyuma wa Ofisi |
![]() |
Upande wa mbele wa jengo la Ofisi na huo msingi mbele yake ndimo utakamopita ukuta wa kanisa lenyewe |
![]() |
Nguvu kazi ya waumini wa kanisa hilo la Overcomers Power Centre zikionekana hapo |