Friday, 25 January 2013

Timu nzima ya Clouds Media Group yaukaribisha mwaka kwa hafla ya kukata na shoka

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group,Bwa.Joseph Kusaga akiwa sambamba na mke wake,ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni bingwa ya burudani hapa nchini,ya Prime Time Promotions Ltd,Johayna Kusaga,akizungumza mbele ya wafanyakazi mbalimbali wa kampuni hiyo waliokutana  kwenye hafla fupi (hawapo pichani) ya kuukaribisha mwaka na kuzungmza mambo mbalimbali ikiwemo na mafanikio yaliyopatikana mwaka jana,pia kuwashukuru kwa ushirikiano wao mkubwa ambao wamekuwa wakionesha kwenye kampuni hiyo kwa ammoja.


 Eprahim Kibonde akimminia kinywaji aina ya Shampeni meneja wa vipindi Sebastian Maganga baada ya kufunguliwa,ikiashiria kuwa hafla ya kunywa,kula imefunguliwa rasmi usiku huu huku baadhi ya wafanyakazi wa Clouds Media wakishuhudia tukio hilo.
 Mtangazaji wa kipindi cha power breakfast,Gerald Hando akizungumza jambo mbele ya Wafanyakazi wenzake usiku huu kabla ya kufungua shampeni,wa pili kulia ni Barbra Hassan,B Dozen,Eprahim Kibonde,Millard Ayo pamoja na Dina Marious.

 
PJ,Suka,Dj Steve B pamoja na Dj Peter Mo wakipata msosi huku wakibadilisha mawazo usiku huu ndani ya kiota cha Escape 2

Shot,Dj Bulla akiw ana Mdau kimapozi ndani ya picha.
 Mmoja wa watangazaji wa kipindi cha Power Breakfast,Paul James a.k.a PJ akifurahia jambo na Meneja vipindi wa clouds FM,Sebastian Maganga usiku huu ndani ya kiota cha maraha cha Escape 2. 

No comments:

Post a Comment