Tuesday, 8 January 2013

SERIKALI KUKAMILISHA UJENZI WA MADARAJA 10 SEHEMU MBALMBALI NCHINI

Wananchi wakivuka kwa taabu sehemu ambako daraja la bonde la Mbutu wilayani Igunga linajengwa na kuondoa kabisa tatizo hilo mwaka huu ambapo ujenzi huo unaofanywa na muungano wa makandarasi wa Tanzania unatarajiwa kukamilika. Mpaka sasa asilimia 45 ya ujenzi wa daraja hili lenye thamani ya sh bilioni 11.28 umekamilika na inakadiriwa kuwa litakuwa tayari ifikapo Novemba mwaka huu.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya jinsi mashimo yatayosimikwa nguzo za daraja hilo yanavyochimbwa
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mawaziri, wabunge na maofisa waandamizi wa wizara na wakala wa ujenzi (TANRODS) pamoja na viongozi wa bodi ya wakandarasi akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa daraja hilo
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine wakipozi na umoja wa wakandarasi wazalendo kutoka makampuni mbalimbali waliopewa kandarasi ya kujenga daraja hilo.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa Serikali yake inakaribia kukamilisha ujenzi wa madaraja yote 10 yaliyoahidiwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na ambayo yanagharimu mabilioni ya fedha.

 Rais Kikwete amesema kuwa kati ya madaraja hayo ambayo thamani yake inakaribia sh. bilioni 415, madaraja mawili tayari ujenzi wake umekamilika. Madaraja hayo ni lile la Ruhekei lililoko Wilaya ya Mbinga katika Mkoa wa Ruvuma na Daraja la Mwatisi katika Mkoa wa Morogoro.
Rais Kikwete amesema kuwa madaraja mengine saba yanaendelea kujengwa, ikiwa ni  pamoja na Daraja la Kigamboni, Mkoa wa Dar es Salaam linalogharimu sh bilioni 214.6, Daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi, Mkoa wa Kigoma unaogharimu sh bilioni 90.185, Daraja la Kilombero, Mkoa wa Morogoro linalogharimu sh bilioni 53.214 na Daraja la Rusumo, Mkoa wa Kagera linalogharimu sh bilioni 31.7.
Madaraja mengine yanayoendelea kujengwa ni Daraja la Sibiti, Singida,  linalogharimu sh bilioni 17.5, Daraja la Nangoo, Mkoa wa Mtwara linalogharimu sh bilioni 4.29 na Daraja la Maligisu, Mwanza, linalogharimu sh bilioni 2.51.

No comments:

Post a Comment