Friday, 25 January 2013

Timu nzima ya Clouds Media Group yaukaribisha mwaka kwa hafla ya kukata na shoka

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group,Bwa.Joseph Kusaga akiwa sambamba na mke wake,ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni bingwa ya burudani hapa nchini,ya Prime Time Promotions Ltd,Johayna Kusaga,akizungumza mbele ya wafanyakazi mbalimbali wa kampuni hiyo waliokutana  kwenye hafla fupi (hawapo pichani) ya kuukaribisha mwaka na kuzungmza mambo mbalimbali ikiwemo na mafanikio yaliyopatikana mwaka jana,pia kuwashukuru kwa ushirikiano wao mkubwa ambao wamekuwa wakionesha kwenye kampuni hiyo kwa ammoja.


 Eprahim Kibonde akimminia kinywaji aina ya Shampeni meneja wa vipindi Sebastian Maganga baada ya kufunguliwa,ikiashiria kuwa hafla ya kunywa,kula imefunguliwa rasmi usiku huu huku baadhi ya wafanyakazi wa Clouds Media wakishuhudia tukio hilo.
 Mtangazaji wa kipindi cha power breakfast,Gerald Hando akizungumza jambo mbele ya Wafanyakazi wenzake usiku huu kabla ya kufungua shampeni,wa pili kulia ni Barbra Hassan,B Dozen,Eprahim Kibonde,Millard Ayo pamoja na Dina Marious.

 
PJ,Suka,Dj Steve B pamoja na Dj Peter Mo wakipata msosi huku wakibadilisha mawazo usiku huu ndani ya kiota cha Escape 2

Shot,Dj Bulla akiw ana Mdau kimapozi ndani ya picha.
 Mmoja wa watangazaji wa kipindi cha Power Breakfast,Paul James a.k.a PJ akifurahia jambo na Meneja vipindi wa clouds FM,Sebastian Maganga usiku huu ndani ya kiota cha maraha cha Escape 2. 

Kamati ya Bunge ya Maliasili na Mazingira yakutana na Watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais

_DSC0391Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa akitoa Maelezo ya Matumizi ya Bajeti ya Nusu  Mwaka wa Fedha 2012/2013 Mbele ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Mazingira Kwenye Ofisi za  Bunge Jijini Dar es Salaam.
_DSC0379 
Wajumbe wa kamati wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dk Tereyza Huvisa  kikao hicho kilichofanyika kwenye ofisi za Bunge Jijini Dar es Salaam

Tuesday, 15 January 2013

LEODGAR TENGA KUTOGOMBEA TENA URAIS TFF


 Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amesema hatagombea tena wadhifa huo katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari 24 mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ofisi za TFF leo, Rais Tenga amesema wakati anaingia kwenye uongozi mwaka 2004 ajenda ilikuwa na kuijenga TFF kama taasisi kwa kuweka mifumo ya uendeshaji ikiwemo kutengeneza katiba na kanuni, jambo ambalo limefanyika. “Wajumbe wamekuwa wakiniuliza Rais vipi? Mimi hapana.

Nilishafika pale pa kufika. Tulipoanza wakati ule ilikuwa ni kujenga taasisi. Na kazi hiyo tumeifanya. Tulipoingia mwaka 2004 hiyo ndiyo ilikuwa ajenda,” amesema Rais Tenga.

 Amesema walitengeneza Katiba, vyombo huru vya kufanya uamuzi, kuongeza wigo wa wapiga kura ambapo hivi sasa kwenye mpira wa miguu hakuwezi kutokea migogoro, hata ikitokea kuna mfumo wa kuidhibiti.

 Rais Tenga ameishukuru Sekretarieti ya TFF, Kamati ya Uchaguzi ya TFF, kamati za uchaguzi za wanachama wa TFF na vyama wanachama wa TFF kwa hatua iliyofikiwa katika uchaguzi ambapo mikoa yote imekamilisha uchaguzi na kubaki vyama shiriki pekee.

Ametoa mwito kwa wadau kujitokeza kugombea uongozi TFF, kwani baada ya kujenga taasisi ajenda iliyobaki ni mpira wa miguu wenyewe ikiwemo nini kifanyika ili mpira uchezwe katika maeneo mbalimbali. “Tumeshatengeza mfumo, sasa ni kuangalia jinsi ya kuendeleza mpira.

 Changamoto ni tufanye nini ili mpira uendelee. Tunataka watu wengine wabebe hiyo ajenda ili tuangalie tunakwendaje mbele,” amesema. Pia amesema ushirikiano ambao amepata kwa wapenzi na wadau wa mpira wa miguu ni wa ajabu. Vilevile ameishukuru vyombo vya habari, Serikali, klabu, wadhamini na wafadhili kwa mchango wao katika uendeshaji wa mpira wa miguu nchini.

19 WACHUKUA FOMU UCHAGUZI TFF Wadau 19 wamechukua fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) unaotarajiwa kufanyika Februari 24 mwaka huu. Fomu hizo zimeanza kutolewa leo (Januari 14 mwaka huu) ambapo wawili wamechukua nafasi ya Makamu wa Rais wakati waliobaki wanaomba ujumbe wa Kamati ya Utendaji wakiwakilisha kanda mbalimbali.

Waliochukua fomu za umakamu wa rais ni Wallace Karia na Ramadhan Nassib. Wote ni wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF inayomaliza muda wake. Waliochukua fomu za ujumbe ni Shaffih Dauda, Athuman Kambi, Hussein Mwamba, Stewart Masima, Yusuph Kitumbo, Mugisha Galibona, Vedastus Lufano, Twahili Njoki, Charles Mugondo, Elley Mbise, Farid Nahdi, Ayubu Nyaulingo, Nazarius Kilungeja, Epaphra Swai, Khalid Abdallah, James Mhagama na Selemani Bandiho.

PONGEZI UONGOZI MPYA KATAVI Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Katavi (KAREFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika jana (Januari 13 mwaka huu).

 Ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa KAREFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo mkoani Katavi

. TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya KAREFA chini ya ukatibu wa Peter Hella aliyeibuka mshindi katika uchaguzi huo uliofanyika ukumbi wa DC mjini Mpanda kwa kumshinda Emmanuel Chaula kwa kura sita dhidi ya mbili.

Uongozi huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu mkoani Katavi kwa kuzingatia katiba ya KAREFA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake. Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya KAREFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.

Viongozi waliochaguliwa ni Hella (Katibu), Elias Mande (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF) na Deo Bakuba (Mwakilishi wa Klabu TFF).

 Nafasi ya Mwenyekiti haikuwa na mgombea wakati Mawazo Maso aliyekuwa mgombea pekee wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti alipata kura nyingi za hapana. Nafasi zilizo wazi zitajazwa katika uchaguzi mdogo. Boniface Wambura Ofisa Habari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

WALIOKUWA ASKARI POLISI MKOA WA KAGERA WAPANDISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA MENO YA TEMBO

IGP Said Mwema Ajiuzulu. Jeshi la Polisi Limekuwa Jeshi la Mauaji



WATUHUMIWA wanne wakiwemo waliokuwa askari polisi kutoka Biharamulo na
Kagera  waliokamatwa na vipande 18 vya meno ya tembo wilayani
Serengeti wamepandishwa kizimbani kwa makosa mawili ya uhujumu uchumi.

Mwandishi   wetu Anthony Mayunga anaripoti kutoka SerengetiWaliofikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya hiyoAmoni Kahimba ni  Boniphace John Kurwa(31)
Gerard Tuti (33) David Delina(36) wakulima wakazi wa Biharamulo na
Bukoba na Zainabu Hamisi Msabaha(26)fundi cherahani mkazi wa
Biharamulo.

Mwendesha mashitaka wa polisi sajenti wa polisi Paskael Nkenyenge
mahakama  iliyofurika wasikilizaji kuwa katika muda ,siku wala tarehe
isiyojulikana watuhumiwa hao walikamatwa kwa kosa la kula njama za
kufanya biashara haramu ya nyara za taifa kinyume na sheria ya kanuni
ya adhabu namba 384(16) iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Alisema watuhumiwa hao na wengine ambao hawajakamatwa Tuguro
Zakayo,Nyarata Mewama,Emanuel Kananjire(Mnyarwanda)ambao wanatafutwa
wanakabiliwa na kosa hilo .

Katika kosa la pili mwendesha mashitaha huyo aliliambia mahakama kuwa
katika kosa la pili kuwa mnamo januari 4,2013 majira ya saa 5 usiku
katika eneo la Morotonga wilayani Serengeti alikamatwa na vipande 18
vya meno ya tembo vyenye uzito wa kg 104 vyenye thamani ya
tsh,66,760,000= kinyume cha sheria.

Alisema kosa hilo ni kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu namba 86
kifungu cha 1,2 cha sheria namba 5 ya mwaka 2009 pia kifungu cha
14(d)cha sheria za uhujumu uchumi namba 60(ii) sura ya 200
iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Kutokana na kosa hilo la uhujumu uchumi mshitakiwa hakutakiwa kujibu
lolote kwa kuwa kosa hilo mpaka wapate kibali cha mwendesha mashitaka
wa serikali(DPP).

Katika kosa la kwanza washitakiwa wote walikana,na mwendesha mashitaka
akaomba siku nyingine ya kutajwa kwa shitaka hilo kwa kuwa upelelezi
haujakamilika na kuwa dhamana .

Hata hivyo mwendesha mashitaka wa polisi Inspekta msaidizi Abdallah
Idd aliyekuwa akishirikiana na Nkenyenge aliomba dhamana izingatie
sheria namba 148 kifungu cha (5)(e)kuwa wadhamini wawasilishe fedha
taslimu zaidi ya tsh,mil.10 au hati ya mali isiyohamishika.

Hata hivyo Hakimu Kahimba alitaka kujua sharti hilo ni kwa washitakiwa
wote ama mmoja,ambapo mwendesha mashitaka Nkenyenge alidai ni kwa
mshitakiwa mmoja Kurwa,madai aliyoyakataa kwa madai kuwa yanawahusu
wote.

Mbali na hilo aliwataka warekebishe mashitaka yao kwa kuwa hayaeleweki
,kwa kutoweka muda na sehemu walikowakamatia inatia shaka ,na kuhoji
wamejuaje wanastahili kushitakiwa Mugumu na si kwingineko.

Akitoa masharti ya dhamana Hakimu Kahimba alisema kila mshitakiwa
anatakiwa atajidhamini mwenyewe kwa dhamana ya tsh,mil.2 ya maneno,pia
mshitakiwa atadhaminiwa na watu wawili wanaoaminika na kueleweka na
wawe wakazi wa Serengeti kwa dhamana ya tsh,mil.10 za maneno.

Sharti la tatu wadhamini ambao ni wakazi wa wilaya hiyo wanatakiwa
kuweka fedha taslimu mil.34 mahakamani ama mali isiyohamishika yenye
thamani ya zaidi ya tsh,mil.35

Na kuwa mali hiyo iwe na hati inayotambuliwa na imefanyiwa uthamini na
mthamini anayetambulika na serikali na wala si barua za watendaji
ambazo amesema zimechangia watu wengi kukimbia kesi zao na
hawaeleweki.

Washitakiwa ,wadhamini na ndugu waliomba mahakama ilegeze masharti kwa
madai kuwa wao ni wageni na hawawezi kuwapata wadhamini wenye sifa
hizo wilayani hapo.

Kabla ya kutoa masharti ya dhamana alitoa angalizo kwa watu
waliojitokeza kuwadhamini washitakiwa hao wakati hawafahamiani na kuwa
watanunua kesi zisizowahusu.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi januari 28 mwaka huu itakapotajwa tena na
watuhumiwa wote wamerudishwa mahabusu baada ya kukosa wadhamini wenye
sifa zilizotajwa na mahakama,na kibali kimetolewa watuhumiwa wengine
watafutwe ili waunganishwe na wenzao.

Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo Tuti na Derina ambao walikuwa
askari upepelezi Biharamulo na Kagera walifukuzwa kazi januari 10,2013
baada ya kupatikana na kosa kijeshi ili washitakiwe kiraia.


  Washitakiwa hao walikamatwa januari 6,mwaka huu katika nyumba ya
kulala wageni baada ya Kurwa kuwataja na kubainika kuwa walikuwa
askari kanzu  kutoka Biharamulo na Kagera ambao ni D/c Gerard Tuti
mwenye namba za F5553 ambaye ni mpelelezi katika ofisi ya kamanda wa
makosa ya jinai wilayani Bukoba .

Askari mwingine ni D/c koplo David Delina mwenye namba E9172 kutoka
ofisi ya upelelezi Biharamulo ambao walikuwa na gari  aina ya Toyota
Ballon lenye namba za usajiri T403 BJK mali ya mtuhumiwa
David.Mtuhumiwa mwingine ni  Boniphace John Kurwa(31) ambaye ni raia
mkazi wa Geita ambaye alikuwa na pikipiki
yenye namba za usajili T784 CCC aina ya Sunlog.

Ambaye akiwa na mwenzake aliyetajwa kwa jina moja la Nyarata akiwa na
pikipiki yenye namba za usajili T 834 BPH Toyo ambaye alitelekeza
pikipiki na mizigo na kutokomea walikuwa wakitokea kijiji cha
Rwamchanga wakiwa na meno hayo ambayo ni sawa na tembo watatu.

Januari 10 mwaka huu askari hao walifukuzwa kazi rasmi baada ya
mashitaka ya kijeshi kukamilika na kubainika kuwa walitenda kosa la
jinai na hatimaye januari 14 mwaka huu wakapandishwa katika mahakama
ya wilaya kujibu mashitaka yanayowakabili..

WAUAWA NA KUZIKWA KWENYE KABURI MOJA


WILAYA YA MOMBA  MBEYA– MAUAJI
  
MNAMO TAREHE 13.01.2013 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KALUNGU KIJIJI CHA IVUNA TARAFA YA KAMSAMBA WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA. 

WATU WAWILI AMBAO NI 1.ERNEST S/O TWINI MOLELA NA MIZINARA D/O MILILO @ MATELA WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA IVUNA WALIUAWA KWA KUPIGWA NA WATU WASIOFAHAMIKA KISHA KUWAZIKA KATIKA KABURI MOJA .


CHANZO NI TUHUMA ZA KISHIRIKINA BAADA YA MAREHEMU HAO KUTUHUMIWA KUWA NI WACHAWI KWA KUMLOGA MAREHEMU NONGWA S/O HUSSEIN MOLELA ALIYEFARIKI DUNIA TAREHE 12.01.2013 MAJIRA YA SA 16:00HRS BAADA YA KUUGUA MUDA MREFU. 

TUKIO HILO LILITOKEA WAKATI WA MAZISHI YA MAREHEMU NONGWA S/O HUSSEIN MOLELA AMBAPO KUNDI LA WATU WASIOPUNGUA KUMI WALIPANDISHA HASIRA NA KUWATUHUMU MAREHEMU HAO KUHUSIKA NA KIFO CHA NDUGU YAO NONGWA S/O HUSSEIN MOLELA HIVYO KUANZA KUWASHAMBULIA KWA KUTUMIA NGUMI, FIMBO NA MAWE KISHA KUWATUMBUKIZA KATIKA KABURI ALILOKUWA AKIZIKWA MAREHEMU NONGWA S/O HUSSEIN MOLELA WAKIWA HAI NA KUWAZIKA WOTE WATATU KATIKA KABURI HILO MOJA. 

BAADA YA HAPO WATU HAO WALIKWENDA NYUMBANI KWA ERNEST S/O TWINI MOLELA NA KUICHOMA MOTO NYUMBA YAKE. KUFUATIA TUKIO HILO WATUHUMIWA WAWILI WALIOKUWA VINARA WA TUKIO HILO WAMEKAMATWA AMBAO NI 1. VENA S/O ERNEST MOLELA [MTOTO WA MAREHEMU ERNEST S/O TWINI MOLELA], MIAKA 26, MUWANDA, MKULIMA NA 2. EMANUEL S/O CHRISTOPHA, MIAKA 16, MUWANDA MKULIMA WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA IVUNA.  MAREHEMU WOTE WATATU NI NDUGU WA UKOO MMOJA. TARATIBU ZA KUFUKUA KABURI ILI MIILI YA MAREHEMU IFANYIWE UCHUNGUZI ZINAFANYWA. 

AIDHA TARATIBU ZINAFANYWA ILI WATUHUMIWA WAFIKISHWE MAHAKAMANI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA  WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE WAHESHIMU NA KUTII SHERIA PASIPO KUSHURUTISHWA. 

PIA ANAIASA JAMII KUACHANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA KWA JAMII IKIWA NI PAMOJA NA KURUDISHA NYUMA MAENDELEO. 

AIDHA ANATOA RAI KWA JAMII/KIKUNDI CHA WATU WENYE KERO/MALALAMIKO,USHAURI ,UJUMBE MAALUM KUTAFUTA NJIA ILIYO HALALI KUFIKISHA KERO,MALALAMIKO,USHAURI ,UJUMBE WAO KWA NJIA YA MAZUNGUMZO BADALA YA KUTUMIA VURUGU/FUJO NA KUSABABISHA MAUAJI.

NAMBA ZA SIMU ZA WAKUU WA POLISI WILAYA/MKOA WA MBEYA


S/NO
                      JINA
CHEO
NAMBA
OFISI/MADARAKA
1.      
CHUMBA CHA MAWASILIANO
0658376007
MBEYA-IPO HEWANI MASAA 24
2.      
MICAH MTAFYA
S/SGT
0755-679488
MKUU WA UPELELEZI (W)MOMBA
3.      
MAJALIWA  MBOGELA
INSP
0754-813368
MKUU WA POLISI JAMII(M) MBEYA
4.      
LAISON N.BUYA
SP
0784-434936
MKUU WA POLISI(W) MOMBA
5.      
LIMITED MUHONGOLE
ASP
0784-205342
MKUU WA UPELELEZI (W)MBARALI
6.      
JULIUS LUKINDO
SSP
0785-264210
MKUU WA POLISI(W) MBARALI
7.      
ROGASIAN L. WENGA
ASP
0767-461055
MKUU WA UPELELEZI (W)KYELA
8.      
JUMA BWIRE
SSP
0754-951464
MKUU WA POLISI (W)KYELA
9.      
ELIAKIM MAGAMBO
ASP
0767-332741
MKUU WA UPELELEZI(W) MBOZI
10.   
GENNYVITUS.V.DUDU
SSP
0784-391402
MKUU WA POLISI(W) MBOZI
11.   
SILVESTER T. IBRAHIM
SP
0754-497402
MKUU WA POLISI (W)RUNGWE
12.   
KISANJO M. PESA
SP
0756-666815
MKUU WA UPELELEZI (W)RUNGWE
13.   
JOSEPH MAFUNDA
ASP
0762-430855
MKUU WA UPELELEZI (W)ILEJE
14.   
ISSA MNILOTA
SSP
0762-265899
MKUU WAPOLISI (W) ILEJE
15.   
GALUS HYERA
ASP
0715-746543
MKUU WA UPELELEZI (W)CHUNYA
16.   
MATIKU
SSP
0754-206495
MKUU WA POLISI (W)CHUNYA
17.   
MTATIRO N. KITIKWI
ASP
0754-615534
MKUU WA UPELELEZI (W)MBEYA
18.   
RICHARD MCHOMVU
SP
0755-816730
MKUU WA POLISI (W )MBEYA
19.   
HENRY NGUVUMALI
ASP
0767-319081
MKUU WA USALAMA  BARABARANI( W)  YA MBEYA
20.   
BUTUSYO MWABELO
SSP
0788-242667
MKUU WA USALAMA BARABARANI MKOA WA MBEYA
21.   
ROBERT MAYALA
SSP
0786-279999
MKUU WA UPELELEZI MKOA WA MBEYA
22.   
DIWANI  ATHUMAN
ACP
0715-009931
RPC