Wednesday, 5 December 2012
TFF yawaangukia wajumbe mkutano mkuu
RAIS wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Leodegar Tenga, amewaomba wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF, wakubali kuridhia mabadiliko ya katiba kwa kupitia waraka, kutokana na umuhimu wa mabadiliko hayo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Tenga alisema TFF imepewa maagizo na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) pamoja na lile ya Afrika (Caf), kuviingiza vipengele vitatu katika katiba.
“Tumeagizwa na Caf kwamba suala la club licence (leseni ya klabu) liingizwe kwenye katiba. Hili suala sisi tulikuwa nalo lakini lilikuwa kwenye kanuni. Sasa Caf imesema lazima tuliingize kwenye katiba na tusipofanya hivyo klabu zetu hazitaruhusiwa kushiriki michuano yoyote ya Caf mwakani.
“Lingine ni suala la uchaguzi. Sisi tuliona hatuna sababu ya kuwa na kamati ya rufaa ya uchaguzi. Tukaona kamati ya rufaa ya kawaida.
Labels:
Michezo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment