Bw. Juma Pinto Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concept (T) Limited kushoto akiwa pamoja na Lightness Sirikwa Meneja Matangazo na na Mhariri Mkuu Yakobe Chiwambo wakionyesha gazeti jipya la matangazo la Dar Metro lililozinduliwa leo katika mgahawa wa City Sports Lounge Posta jijini Dar es salaam jioni ya leo, ambapo wadau kutoka makampuni mbalimbali yanayojihuzisha na biashara ya matangazo wamehudhuria katika hafla hiyo, gazeti hilo litagawiwa bure katika maeneo mbalimbali ya kibiashara jijini Dar es salaam na mikoani hapa nchini
Bw. Juma Pinto Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concept (T) Limited akizungumza na wageni waalikwa wakati alipozindua rasmi gazeti la matangazo linaloitwa Dar Metro kwenye mgahawa wa City Sports Posta jijini Dar es salaam, katikati ni Peter Ambilikile Mwandishi mwandamizi wa gazeti la Dar Metro na kulia ni Lightness Sirikwa Meneja Matangazo wa gazeti la Dar metro
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts (T) Limited Mzee Ramadhan Kibanike akizungumza katika uzinduzi huo

No comments:
Post a Comment