Tuesday, 11 December 2012

MKUU WA MKOA WA RUKWA AFANYA ZIARA KUHAMASISHA KILIMO BORA NA SHUGHULI MBALIMBALI ZA MAENDELEO MKOANI HUMO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na umati mkubwa wa wananchi wa kata ya Mao waliojitokeza kumsikiliza kwenye mkutano wa hadhara akiwa ziarani Mkoani Rukwa kuhamasisha kilimo na shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwepo chanjo ya minyoo na vitamin A kwa watoto walio chini ya miaka mitano, elimu, utawala bora na kampeni ya ondoa nyasi weka bati ijulikanayo kama “Onyaru” Ondoa nyasi Rukwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akizungumza na wananchi wa kata ya Legezamwendo Wilayani Kalambo katika ziara yake ya kuhamasisha kilimo bora na shughuli mbalimbali za maendeleo. Katika kata zote 13 alizotembelea wananachi walijitokeza kwa wingi ambapo pia walipewa fursa ya kuuliza maswali na kuwasilisha kero zao. Maswali na kero zao zilipatiwa ufumbuzi na nyingine kupewa muda kushughulikiwa.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na wananchi wa Kata ya Mshani kwenye ziara yake ya kuhamasisha kilimo na shughuli mbalimbali za kimaendeleo Mkoani humo. Wananchi wengine walilazimika kupanda juu ya miti ili kuweza kupata ujumbe vizuri.
Ziara hii ya Mkuuu wa Mkoa wa Rukwa wa Rukwa ilienda sambamba na zoezi la chanjo ya minyoo na vitamin A kwa watoto waliochini ya miaka mitano. Pichani ni Dkt. Edina Yesaya ambaye ni kaimu mganga mkuu wa Halamashauri ya Wilaya ya Sumbawanga akitoa chanjo kwa mmoja ya watoto waliofika kupata chanjo hiyo. Watoto zaidi ya 2000 wamepata chanjo hiyo katika kata na vijiji 13 msafara huo ulipopita.
 
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Ndugu Moshi Chang’a akisisitizia jambo kwa wananchi wa kata ya Kilembe. Aliwataka wananchi kwa kushirikiana na uongozi wa kata na watendaji kushirikiana kuhakikisha miundombinu katika shule ya Msingi Kilembe inaboreshwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Ndugu Moshi Chang’a akimkaribisha kwa shangwe Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ili aweze kuzungumza na wananchi wa Kata ya Legezamwendo katika ziara yake ya kuhamasisha kilimo bora na shughuli mbalimbali za maendeleo.
Muimbaji wa kikundi cha kwaya cha Last kutoka Kata ya Legezamwendo akiimba kwa staili ya aina yake huku akisalimiana na viongozi waliokuwepo meza kuu. 
Mambo yalikuwa hivi katika makao makuu ya Wilaya mpya ya kalambo. Wananchi walifurika kwa wingi. Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliwata viongozi na wananchi wa Wilaya hii mpya kuzingatia kujenga mji wao kwa kuzingatia mipango miji iliyo bora pamoja na kusisitizia suala la usafi ambapo Mkuu wa Wilaya hiyo Ndugu Moshi Chang’a ameteua siku ya jumamosi ya kila wiki kuwa siku ya usafi kwa Mji mzima wa Matai ambao ndio makao makuu ya Wilaya ya Kambo.
 Wananchi walipewa fursa ya kuuliza maswali na kutoa kero zao.
 
Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Kalambo Bwana Ngindo akifurahia jambo na Kaimu Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Bwana Frank Mateni na Afisa Kilimo kwenye dawati la uwekezaji Bwana Misasi Marco kwenye ziara hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na madereva wa bodaboda katika Mji mdogo wa Laela katika ziara yake Mkoani Rukwa ya kuhamasisha kilimo bora na shughuli nyingine mbalimbali za kimaendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akigawa “Reflectors” kwa madereva wa bodaboda katika Mji mdogo wa Laela uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ambapo anafanya ziara katika Mkoa huu kuhamasisha kilimo bora katika msimu huu wa kilimo pamoja na shughuli nyingine za kimaendeleo. Mkuu huyo wa Mkoa aliwaasa vijana hao kujenga umoja wenye nguvu kwani utawasaidia pia kupata mikopo mbalimbali. Aliugiza uongozi wa halmashauri kuwapimia viwanja madereva hao ambao wapo 22 viwanja ambavyo watavilipia wao wenyewe. 
Zaidi ya asilimia 70% ya wakulima Mkoani Rukwa hutumia jembe la kukokotwa na wanyama katika shughuli zao za kilimo. Mkulima katika kijiji cha Matanga akiandaa shamba lake kwa ajili ya kupanda mazao katika msimu huu mpya wa kilimo cha mvua wa mwaka 2012.
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Ndugu Moshi Chang’a akiwaimbisha wananchi wa Kata ya Kilembe Wilayani Kalambo ikiwa ni kuwaweka sawa kwa ajili ya kumsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliyepo kwenye ziara ya kuhamasisha kilimo bora na shughuli pamoja na miradi mbalimbali ya maenedeleo.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa – rukwareview blog)

MZEE MSTAAFU WA USALAMA WA TAIFA AUWAWA KWA KUKATWA NA MAPANGA MBEYA HUYU HAPA.


MAREHEMU JOSEPH MWASOKWA AMEUWAWA JANA USIKU MAJIRA YA SAA MBILI NA NUSU USIKU NJE YA NYUMBA YAKE 
MZEE JOSEPH MWASOKWA  AKIWA NARAFIKI YAKE NA NDIYO WALIOKUWAWOTE JANA USIKU WAKITOKEA KUANGALIA MECHI ZA BARA LA ULAYA  WAKAAGANA VIZURI TU NA MZEE MWASOKWA AKAWA ANAELEKEA KWAKE NA NDIKO MAUTI YALIMKUTA KWA KUKATWA NA MAPANGA
HAPA NDIPO WALIPOMUULIA MZEE MWASOKWA NJE YA NYUMBA YAKE JANA USIKU
ADRIAN MAGEMBE MWENYEKITI WA MTAA WA BLOCK T ALIKOKUWA ANAISHI MAREHEMU AKITUELEZEA JINSI ALIVYOPATA TAARIFA YA MSIBA WA RAFIKI YAKE MPENDWA AMESEMA MZEE MWASOKWA ALIKUWA KIPENZI CHA WENGI KATIKA ENEO HILO LA BLOCK T ANASHINDWA KUELEWA HAWA WATU WALIOMUUA WALIKUWA NA KISA GANI MAANA VITU VYOLE WALIMKUTANAVYO KAMA SIMU POCHI NA VITU VINGINE WAUAJI HAWAKUONDOKA NA KITU CHOCHOTE
MHESHIMIWA MBUNGE WA MBEYA MJINI JOSEPH MBILINYI NAE ALIKUWEPO HAPO MSIBANI KUWAFARIJI WAFIWA AMESEMA AMESIKITISHWA SANA NA KIFO CHA WAJINA WAKE MZEE MWASOKWA YEYE HANA LA KUSEMA ZAIDI KAZI TUWAACHIE WANAUSALAMA WAFANYE KAZI YAO
MPOKI MTOTO WA MAREHEMU YEYE NDIO ALIKUWA WA KWANZA KUUONA MWILI WA BABA YAKE HAPO NJE ASUBUHI YA LEO
MAREHEMU MZEE JOSEPH MWASOKWA ALIKUWA MWANACHAMA WA YANGA. NA MBEYA YETU BLOG. 

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA( TCRA) WAPO MKOANI MBEYA KUPIMA MIONZI YA MINARA YA MAWASILIANO

Baadhi ya wataalamu toka mamlaka ya mawasiliano Tanzania wakiwa katika kupima kiwango cha mionizi ya minara ya mawasiliano mkoani Mbeya hapa ni eneo la ofisi za jiji la mbeya

Hii siyo Mic yaani cha kusemea bali ni moja ya vifaa vya kupimia mionzi ya minara ya mawasiliano hapa nchini





KAMPUNI YA AIRTEL YAANZA SHAMRA SHAMRA YA CHRISTMAS


Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sam Elangalloor (katikati), akizungumza na mmoja wa wateja mashuhuri wa kampuni hiyo, Jaji Joaquine Antoinette De-Mello(kushoto) katika onyesho maalumu la muziki la Christmas la kwaya ya Dar Choral Society  lililodhaminiwa na Airtel katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Wateja wa Makampuni wa Airtel. Irene Madeje.
Kikundi cha kwaya cha Dar Choral Society kikitumbiza katika onyesho maalumu la muziki la Christmas la kwaya hiyo  lililoandaliwa na  Airtel kwa wateja wao wa makampuni  katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam jana.
Father x-mas akitoa zawadi kwa mmoja wa watoto waliohudhuria onyesho maalumu la muziki la Christmas la kwaya ya Dar Choral Society lililoandaliwa na  Airtel kwa wateja wao wa makampuni  katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya wanamuziki wa Kikundi cha kwaya cha Dar Choral Society wakionyesha umahiri wao katika onyesho maalumu la muziki la Christmas la kwaya hiyo  lililoandaliwa na  Airtel kwa wateja wao wa makampuni katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Wateja wa Makampuni wa Airtel, Irene Madeje (wa pili kushoto) akizungumza na baadhji ya wateja wokatika onyesho maalumu la muziki la Christmas la kwaya ya Dar Choral Society   lililoandaliwa na  Airtel kwa wateja wao wa makampuni  katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya watu waliohudhuria onyesho maalumu la muziki la Christmas la kwaya ya Dar Choral Society  lililoandaliwa na  Airtel kwa wateja wao wa makampuni  katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam jana.

Thursday, 6 December 2012

HARUSI YA FESTO NA ELIZABETH YAFANA JIJINI MBEYA


Bwana Festo Ngonela  ni mtumishi wa CRDB BANK na Bi Elizabeth Malimbwi yeye ni mwalimu Mbalizi wakiwa mwili mmoja sasa mara baada ya kufunga ndoa katika kanisa la mtakatibu Anthon wa paua jijini mbeya
Bi harusi akimvisha pete mumewe kuwa mili mmoja
Bwana Festo na Bi Elizabeth wakiwa na nyuso za furaha katika ukumbi wa Rehema jijini Mbeya
Wakiwa na wapambe wao ukumbini hapo
Maharusi wakiwa katika picha ya pamoja na kamati nzito ya harusi yao
Hakika wamependeza maharusi wetu.

VYANDARUA VYATUMIKA KUSAFIRISHIA CHUPA CHAKAVU MBEYA


Chupa chakavu zikiwa zimefungwa vizuri katika vyandarua tayari kwa kusafirishwa kwenda DSM

Sisi hatuna maneno tumejionea wenyewe na wewe ona sasa toa maoni yako



Bonge la mzigo limefungwa kisawasawa tayari kwa kusafirishwa



Chandarua kazini.

VIJANA WA MJI MDOGO MBALIZI MBEYA WILAYANI MBEYA VIJIJINI WAFANYA USAFI WA KUZIBUA MIFEREJI NA KUTENGENEZA BARABARA


Vijana wa Mji mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani Mbeya leo wamefanya kazi ya kufagia kuzibua mifereji na kutengeneza barabara kivutio kikubwa kilikuwa kwa kina dada kwani walijitokeza kwa wingi na kuchapa kazi sambamba na kaka zao
Hakika vijana wa Mbalizi tuwape pongezi kwa kazi nzuri wanayoifanya kwani ni vijana wachache sana wanaojitolea kufanya kazi hizo za usafi wa kujitolea

Vijana hao wa mbalizi wamesema si vema kila kitu kuiachia serikali waka kazi nyingine tunaweza fanya kama hizi za usafi na kutunza mazingira hapa vijana wakipeana mikakati ya kuboreza mjiwao wa mblizi kwa usafi
Hakika ina pendeza mweshimiwa diwani kata ya utengule usongwe ambae pia ni mwenyekiti wa kijiji cha Mbalizi mwenye koti la kijani Mh. Eliah Mkono na mkuu wa kitengo cha kinga na tiba Mbeya vijijini  Emanuel Mwaigugu wakifurahia baada ya kuona vijana wamejitokoza kwa wingi kusafisha mji wao wa mbalizi
Mweshimiwa diwani akikagua kazi inayoendelea ya kuzibua mifereji na kutengeneza barabara
kazi inaendelea

Mweshimiwa diwani hakuwa nyumba katika kuwasaidia vijana 
Kwenye kazi utani pia upo ili kazi iende vizuri dada na kaka wanataniana
Safi sana vijana wa Mbalizi
Mratibu wa Vijana wazalendo wa mji wa Mbalizi Gordon Kalulunga,akiwa na kiongozi mwenzake wakifurahia jinsi kazi inavyoendelea
Hali halisi ya mifereji ya mbalizi ni hii sasa vijana ndiyo wanaizibua
Baada ya kuzibuliwa  kwa ujumla mbeya yetu tunawapongeza sana vijana wa mbalizi kwa umoja wenu tunaomba na vijana wengine muige mfano huo wa kujitolea kufanya usafi zoezi la usafi litaendelea kesho.Picha na Mbeya Yetu