Thursday, 18 July 2013

Kampuni ya Airtel yazima laini za simu zisizosajiliwa 200,000 ili kuongeza usalama Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Bi Beatrice Singano
Airtel yazima laini za simu zisizosajiliwa 200,000 ili kuongeza usalama Dar es Salaam, Tanzania 18 Julai 2013, Airtel Tanzania imetangaza itetimiza tamko la serikali la kuzima laini za simu ambazo hazijasajiliwa ikiwa ni utekelezaji wa sheria ya posta na mawasiliano ya kielektroniki ya mwaka 2010 na  muda wa hitimisho wa kusajili namba uliowekwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)  wa tarehe 10 Julai 2013
 Usajili wa namba ni mchakato wa kuhakiki na kuweka kumbukumbu za mtumiaji wa namba ya simu unaowekwa na mtoa huduma za mawasiliano ya simu, maelezo ya usajili ni pamoja na namba ya simu, tarehe ya kuzaliwa, jinsia, sanduku la posta, namba nyingine ya simu kama ipo, kitambulisho na namba ya kitambulisho kilichowakilishwa

Akiongea kwa niaba ya Airtel , Mkurugenzi wa Mawasiliano na Usimamizi wa Sheria Beatrice Singano alisema" wateja wetu wote walijulishwa mapema kusajili simu zao na tumetoa muda wa kutosha kwa zoezi hili la usajili kufanyika ili kuepuka kufungiwa simu zao.  Tumetimiza sheria kama inavyosema ya EPOCA na kufunga simu zote ambazo hazijasajiliwa
kuanzia usiku wa tarehe 10 julai kama mamlaka ya mawasiliano ilivyowatangazia mwezi wa April mwaka huu, kwa sasa jumla ya wateja wetu 200,000 tumewafungia mawasiliano kwa kutotimiza tamko hili la kusajili namba zao za simu za Airtel

Tunaamini kwa kufungia simu hizi kuna wateja watabaki bila mawasiliano hivyo tunachukua nafasi hii kuwaomba  wateja ambao hawajasajili simu zao kufanya hivyo  katika vituo vyetu vya huduma ikiwemo,  maduka yetu ya Airtel, wauzaji wa bidhaa zetu wa rejareja na  mawakala wetu wote nchi nzima. Pia kwa wateja wanaonunua namba mpya kuanzia sasa wasajili namba zao ili waweze kuzitumia. Pamoja na hilo pia tunawashauri wateja waliosajiri kuhakiki usajili wao kwa kupiga*106#. Tunaamini zoezi la
usajili litasaidia kudumisha Amani na usalama wa watanzania na zaidi ya yote kukuza sekta ya mawasiliano.

Usajili wa namba za simu umekuwa ukiendelea kwa miaka michache katika ukanda wa jumuiya ya Afrika mshariki (EAC)  ikiwa na lengo la kudhibiti matukio yanayofanyika kwa kutumia namba zisizosajiliwa ikiwemo, wizi kwa njia ya mtandao, utekaji, ujumbe wa matusi, ugaidi na mengine mengi

Kenya na Tanzania imepiga hatua na kufikia zoezi la kuzima simu nchi nyingine za jumuiya ziko katika atua ya awali za utekelezaji, Uganda iko katika hatua ya utekelezaji wa usajili wa namba za simu.

Duniani kote mtumiaji wa simu anatakiwa kusajili simu kadi yake mpaka pale itimisho linapotokea . na mteja yoyote anayeshindwa kusajili simu yake mpaka muda wa hitimisho simu yake itafungiwa na mteja atapoteza namba yake, hivi karibuni usajili wa namba umeendelea katika nchi za Ghana, Sierra Leone Nigeria, Zimbabwe, South Africa, Kenya, Singapore,
Malaysia, Geneva, India, Egypt na nchi nyingine 

Singano amewakumbusha mawakala na wasambazaji wa Airtel kutimiza agizo hili na kuhakikisha kuwa simu kadi yoyote inayouzwa au kupewa mteja iwe imesajiliwa kabla ya matumizi, ni kosa la jinai kutumia simu kadi isiyosajiliwa

"Mchakato huu ni wa lazima chini ya sheria ya posta na mawasiliano ya kielektronikia (EPOCA) ya 2010 inayotoa jukumu la muuzaji au mtumiaji wa simu kusajili namba zao kabla ya kuitumia. Na usajili wa namba katika vituo vyetu vya wasambazaji mawakala nchini nzima ni bure aliongeza Singano

chini ya kifungu cha 130 cha sheria ya posta na mawasiliano ya kielektronikia (EPOCA) ya 2010  ni marufuku kwa mtu yeyote kuuza namba ya simu kwa mtu yeyote bila kuweka kumbukumbu za mtumiaji wa namba hiyo.

Thursday, 11 July 2013

MWANAMKE ALIYETUPA MTOTO CHOONI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 5 JELA MKOANI MBEYA


Rukia Haruna (31) akitolewa nje ya mahakama na askari  kwenda gerezani kutumikia kifungo cha miaka mitano.…
Rukia Haruna (31) akitolewa nje ya mahakama na askari  kwenda gerezani kutumikia kifungo cha miaka mitano.
Pichani juu ni taswira za wananchi wa eneo la Manga A jijini Mbeya wakati wakijaribu kuokoa maisha ya kichanga  kilichotupwa chooni na Rukia Haruna Juni 14 mwaka huu.
Picha iliyozibwa ni ya kichanga kilichotupwa baada ya kutolewa chooni.

Mwanamke Rukia Haruna (31), mkazi wa Manga A Jijini Mbeya, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kutupa mtoto wake chooni.
Tukio hilo lilitokea Juni 14, mwaka huu katika eneo hilo baada ya watoto waliokuwa wakicheza kugundua kuwepo kwa mtoto katika choo cha shimo.
Mtuhumiwa baada ya kukamatwa amekiri kutenda kosa hilo na kwamba alifanya hivyo baada ya mzazi mwenzie kumkataa.
Ameongeza kuwa alilazimika kutupa kichanga hicho katika choo cha jirani kwa sababu ni cha shimo tofauti na chao ambacho asingeweza kutupa mtoto huyo.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa, mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Zabibu Mpangula, amemhukumu mtuhumiwa kifungo cha miaka mitano baada ya kosa hilo ambalo ni kinyume cha kifungu  218 kifungu kidogo cha 35 sura ya 16 ya mwaka 2002.
HABARI NA MBEYA YETU BLOG

RAIS JK AFUNGA KONGAMANO LA KITAIFA KUJADILI AMANI

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya kufunga Kongamano la Kitaifa Kujadili Amani ya Taifa lililofanyika katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salam  Jana jioni.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya kufunga Kongamano la Kitaifa Kujadili Amani ya Taifa lililofanyika katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam jana jioni.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Centre for Democracy (TCD) ambaye pia ni kiongozi wa chama cha NCCR Mageuzi Mhe. James Mbatia akimkabidhi Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete maazimio ya Kongamano la Kitaifa kujadili Amani ya Taifa lililofanyika katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam na kufungwa  Jana jioni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wa vyama vya siasa vilivyoshiriki katika Kongamano  la kitaifa Kujadili Amani ya Taifa lililofanyika katika Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.Kushoto ni kiongozi wa Chama cha NCCR Mageuzi Mhe.James Mbatia (MB), Mwenyekiti wa TLP Mhe.Augustine Lyatonga Mrema(watatu kushoto) na kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha UDP Mhe.John Momose Cheyo
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(aliyekaa katikati) Akiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa na washiriki wa Kongamano la Kitaifa Kujadili Amani ya Taifa lililofanyika katika Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.
                                       (PICHA NA FREDDY MARO)