Tuesday, 23 April 2013

BREAKING NEWSSS MWENYEKITI WA UMOJA WA SACCOS TAIFA NA PIA NI MFANYAKAZI WA TAZARA MBEYA AMBROSE LUCAS SHAYO APIGWA ATESWA NA KUCHOMWA MOTO.

HAPA NDIPO ALIPOTESWA NA KUUWAWA AMBROSE SHAYO
HAPA NDIPO ALIPOCHOMWA MOTO NA WATU WASIOJULIKANA

HILI NDILO ENEO GARI YAKE ILIPINDUKA NA WAUWAJI WALIPOPATA NAFASI YA KUMUUA AMBROSE
HAPA NDIPO GARI YA AMBROSE ILIPOGONGA NA KUPINDUKA WAKATI ANAKIMBIZWA NA WAUWAJI HAO

HABARI KAMILI YA TUKIO HILI TUTAZIDI KUWAJULISHA KWANI  POLISI WANAENDELEA NA KAZI YAO. NA MBEYA YETU BLOG.

Monday, 22 April 2013

MWONEKANO MPYA WA GAZETI LA MWANANCHI MBEYA, PATA PICHA HALISI ZA TUKIO ZIMA.


Mkurugenzi Mtendaji wa MCL Tido Mhando akizungumza na wadau mbali mbali jijini Mbeya katika sherehe ya kutangaza mwonekano mpya wa gazeti la Mwananchi
Mkuu wa wilaya Mbeya akiwapongeza wafanyakazi wa MCL kwa kuwahabarisha wananchi kote nchini 
Wadau na wafanyakazi wa Mwananchi wakiangalia makala fupi toka lilivyo anza gazeti la mwananchi mpaka sasa kwenye mwonekano mpya
Baadhi ya waandishi wa MCL
Wadau mbali mbali wakisherehekea mwonekano mpya wa gazeti la mwananchi

Friday, 19 April 2013

WAANDISHI WA HABARI MKOANI MBEYA WATOA ZAWADI KWA WATOTO WA KITUO CHA CHIRD SUPPORT TANZANIA

Mtendaji Mkuu wa Elimisha, Festo Sikagonamo akimkabidhi zawadi moja ya watoto wa kituo cha Chird support Tanzania 
Festo Sikagonamo akiwakabidhi zawadi za watoto kwa viongozi wa chird support 
Baadhi ya waandishi wa habari walioandamana na asasi hiyo ya Elimisha wakigawa zawadi kwa watoto hao 
Danny Tweve moja ya viongozi wa asasi hiyo ya Elimisha akimpatia moja ya watoto zawadi kituoni hapo
Hakika watoto wamefurahi kupata zawadi 
Mtoto mlemavu wa miguu na mikono akionyesha jinsi zawadi yake ya kalamu aliopewa atakavyo andikia
Watoto wakiimba kwa furaha kuwakaribisha wageni wao
Baadhi ya waandishi wa habari walioandamana na asasi ya Elimisha wakiwa makini kuwasikiliza watoto walipokuwa wakiimba
Baadhi ya walimu wa kituo hicho wakiimba pamoja na watoto wao
Mtendaji Mkuu wa Elimisha, Festo Sikagonamo amesema zawadi hizo walizotoa kwa watoto hao wamepata toka kwa wafadhiri mbali mbali
Mkurugenzi wa kituo cha chird support Noera akiwashukuru asasi ya Elimisha pamoja na waandishi wa habari kuguswa juu ya watoto anaowalea hapo kituoni kwa kuwapatia zawadi mbalimbali 

MICHEZO YA MEI MOSI KITAIFA YAZINDULIWA MBEYA



Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa mbeya Ndugu   Costantine Mushi.
mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa mbeya Ndugu   Costantine Mushi. akizindua michuano hiyo



Michuano ya mei mosi kitaifa katika uwanja wa kumbukumbu sokoine jijini mbeya imeendela kushika ambapo hii leo michezo mbalimbali imefanyika uwanjani hapo  baada ya kufunguliwa rasmi na mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa mbeya Ndugu   Costantine Mushi.

Katika michezo ya awali kwa upande wa wanaume ilikuwa ni kati ya Wizara ya Mambo ya ndani pamoja na Wizara ya Mali asili.
Matokeo ya mchezo huo Timu ya Mambo ya Ndni imefanikiwa kuibuka kidedea kwa kuicharanga goli 3 kwa mbili timu pinzani.
Katika dk ya 22 maliasili walifanikiwa kuandika bao la kwanza kupitia kwa mchezaji wao Hamisi Changánda mara baada ya kupkea pasi kutoka wingi ya kulia.

 Katika kpindi hicho cha kwanza wapinzani wao ambao ni Mambo ya ndani walisawazisha bao hili katika dk 38 kwa mchezaji westoni mwanjala kwa kichwa ambapo mpaka mchezo huo unakamilika katika kipindi cha kwanza  timu zote zilikwenda suruhu.
Hata hivyo kipindi cha pili mpambano ulikuwa mkali kwani timu zote zilikuwa na kasi kubwa kwani dk ya .47 Andrew Bundara wa mambo ya nadani aliandikia timu yake bao la pili ambapo katika dk ya 60  Hamisi Nyagawa aliipachikia timu yake ya Maliasili bao la kusawazisha.

Mambo ya ndani waliendela kulindama lango la wapinzani wao na kufanikiwa kuandika bao la 3 na la ushindi kupitia kwa mchezaji wao hatari Westoni Mwanjala ambaye nfdite aliyekuwa kinara wa mapmbano huo kwa kuiandikia timu yake ya mambo ya ndani bao 3 katika kipindi chote cha dk 90 za mchezo.
Michezo mwingi ne wa pete kati ya CDA ya Dodoma pamoja Hazina Dar es salaam matokeo ni ,,,,,,,,,,,,CDA 31 Hazina 12…………Ulinzi ya Dar 38 Uhamiaji 17 .
Katika mchezo wa kuvuta kamba Hazina wanaume walishindwa nguvu na Uhamiaji.