Friday, 20 September 2013

KAMPUNI YA SIMU YA AIRTEL YASHIRIKIANA NA TRA KUWAWEZESHA WATEJA KULIPIA ADA ZA LESENI ZA MAGARI.

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Malipo ya Kodi  na Elimu TRA Mrs.Diana Masalla (wa pili kushoto) akifatiwa na Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, ASP Mohamed Mpinga na  Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba kwa pamoja wakizindua huduma itakayowawezesha wateja wa Airtel kulipia ada za leseni ya magari kupitia huduma ya Airtel money wakishuhudia kulia ni meneja kitengo cha Airtel money John Ndunguru , mwisho kushoto ni mwakilishi wa max malipo Tumsifu Lema

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, ASP Mohamed Mpinga akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma itakayowawezesha wateja wa Airtel kulipia ada za leseni ya magari kupitia huduma ya Airtel money pichani kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Malipo ya Kodi  na Elimu TRA Mrs. Diana Masalla (kulia) Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Malipo ya Kodi  na Elimu TRA Mrs.Diana Masalla (wa pili kushoto) akifatiwa na Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, kwa pamoja wakizindua huduma itakayowawezesha wateja wa Airtel kulipia ada za leseni ya magari kupitia huduma ya Airtel money

 Airtel yashirikiana na TRA kuwawezesha wateja kulipia ada za lesseni za magari
Airtel Tanzania kwa kushirikiana na mamlaka ya mapato Tanzania TRA wamezindua rasmi huduma ya kufanya malipo ya ada za  leseni za magari kupitia huduma ya Airtel money. Huduma hii inapatikana bure kwa wateja wote wa Airtel nchi nzima. Hii inawawezesha watumiaji wa huduma hii kulipia leseni ya magari yao wakiwa ofisini au majumbani mwao kwa urahisi zaidi ambapo kwa sasa ni BURE.

Adriana Lyamba, Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel amesema " huduma ya kulipia leseni ya magari kupitia Airtel money imeleta unafuu kwa wateja watakaotaka kulipia leseni za magari. Huu ni mwendelezo wa mapinduzi ya huduma za kifedha kupitia huduma ya Airtel money inayomuhakikishia mteja uharaka, unafuu, usalama na urahisi zaidi katika kulipia huduma mbalimbali. Tunaamini huduma hii ya kulipia leseni za magari kupitia Airtel money kutaleta ufanisi ni kuendeleza juhudi za serikali katika ukusanyaji wa kodi. 
Tunaahidi kuendelea kuleta suluhisho katika huduma za malipo mbalimbali na kuwahakikishia wateja wetu urahisi, usalama na ufanisi zaidi kupitia Airtel Money."

Sasa tumewawezesha wateja wote wa Airtel kulipia leseni za magari bila kuwa na haja ya kutembelea ofisi za TRA kufanya malipo. Wateja watatakiwa kwenda kuchukua leseni/stika zao pale malipo yatakapofanyika na leseni/stika zao kuwa tayari

Akiongea kuhusu huduma ya malipo ya ada za leseni Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Malipo ya Kodi na Elimu TRA Mrs. Diana Masalla alisema" huduma hii mpya inahusisha malipo ya ada za lesseni za magari, ada za uamisho wa magari pamoja na malipo mengine ya ada za usajili wa magari. Huduma hii itawezesha ukusanyaji wa malipo ya ada / kodi zifanyike kwa njia rahisi na nafuu. Unaweza kupata kiasi cha kulipia ada unayotakiwa kulipia kisha ukalipia hapohapo ndani ya sekunde chache kupitia huduma ya Airtel money.  
Ulipaji huu unaenda sambamba na kauli mbiu ya TRA ya Urahisi, Uhiari na Uboreshaji Endelevu Akiongea juu ya namna ya ulipiaji ada Meneja wa kitengo cha Airtel money John Ndunguru alisema" huduma hii inapatikana kwa wateja wa malipo ya awali na ya mwezi.
Aliongeza kwa kusema ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hii, Airtel imeweza kuiweka kwenye MENU ya Airtel Money "TRAMAGARI" ili kuweza kurahisisha ulipaji wa ada na kuiwezesa serikali  ukusanya ada kwa gharama nafuu zaidi"

Kwa upande wake Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, ASP Mohamed Mpinga alisema "Ninawapongeza sana kampuni ya Airtel Kupitia huduma yake ya Airtel Money kwa kushirikiana na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)  kurahisisha ukusanyaji wa kodi hii ya Ada za magari maarufu kama Road License. Hi ni huduma nzuri inayosaidia watanzania kuokoa muda wao pale wanapoweza kutumia simu zao kupitia mtandao wa  Airtel kulipia Ada ya magari yao kila mwaka bila usumbufu."

Kwa urahisi huu inatusaidia sana kuokoa muda ambao ungepotea kukaa kwenye foleni ya malipo na badala yake muda tunaookoa tutautumia katika shughuli nyingine za kiuchumi 
Naomba niwakumbushe kuwa wiki ya usalama barabarani itaanza wiki ijayo tarehe 23.9.2013 hivyo mambo yote ya ukaguzi wa stika za ada za magari yaani (Road Licence) pamoja na Stika za usalama barabarani na ukaguzi wa vyombo vyote vya moto utaenda sambamba, hivyo ninawakumbusha watumiaji wote wa vyombo vyote vya moto kufuata sheria zote zilizowekwa ili kuepuka adhabu ya kulipa faini.

Huduma ya Airtel money inawawezesha wateja kutumia simu zao za mkononi katika huduma za kifedha zikiwemo  kulipa bill ya maji DAWASCO, kulipia Luku TANESCO malipo ya DSTV, kulipia visa ya USA na sasa ada za lesseni ya magari. Airtel money ni huduma rahisi na salama inayotoa huduma za mobile benki na za malipo mbalimbali.

HABARI: KWA HALI HII ZAO LA PAMBA LITAZIDI KUPOROMOKA KILA KUKICHA.

Meneja wa kiwanda cha Bilchand Oil Mill, Mohamed Gupta akifafanua uchafuzi unaofanywa na baadhi ya wanunuzi na wakulima kwa kuchang’anya pamba, maji, mchanga na mbegu kwa lengo la kuongeza uzito.
Ziara ya Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba nchini DKT.FESTUS LIMBU katika kiwanda cha kuchambua pamba cha Birchand Oil mill inayomwezesha kujionea uchafuzi wa pamba unaofanywa na baadhi ya wanunuzi na wakulima kwa kuchang’anya pamba, maji, mchanga na mbegu kwa lengo la kuongeza uzito.
Mbegu zilizochanganywa kenye pamba kwa lengo la kuongeza uzito
Ukaguzi ukiendelea kwenye ghala la Pamba.
Meneja wa kiwanda cha Bilchand Oil Mill, Mohamed Gupta akionyesha mchanga uliochanganywa na Pamba za moja wa wakulima waliokiuzia kiwanda chake.
Ukiitizama kwa harakaharaka pamba hii unaweza kuiona kuwa iko salama, ila ukichukuwa jukumu la kuigusa ndipo utagunduwa kuwa kunachembe chembe za mchanga na uchafu mwingine ndani yake.
Hili ni lundo la mchanga wa kilo 60,000 uliopembuliwa wakati wa uchambuzi wa pamba ya msimu huu na uliopita, kwa Kiwanda cha Bilchand Oil Mill ambacho kimepata hasara ya zaidi ya shilingi milioni 7 kutokana na uchafuzi huo wa kuweka maji na mchanga, hadi sasa Wahasibu wake wanne (hakuwataja) wafikisha polisi kwa tuhuma hizo.  
Meneja wa kiwanda cha Bilchand Oil Mill, Mohamed Gupta akielezea uchafuzi huo ndani ya Pamba.
Kwa ukaribu zaidi mchanga uliopatikana kwenye Pamba baada ya uchambuzi wa awali.

Na Peter Fabian
MWANZA.
TATIZO la kushuka thamani ya Pamba nyeupe ya Tanzania (Dhahabu Nyeupe) kwenye Soko la Dunia na kupelekea kuporomoka kwa bei maradufu kumeishitua seikali na sasa kupitia Bodi ya Pamba nchini (TCB)imeamua kuchukua hatua za kunusuru zao hilo kwa kutangaza kuwa kuanzia msimu ujao wa kilimo utakuwa wa Kilimo cha Mkataba katika Mikoa ya Kanda ya Magharibi.
Hatua hiyo inafuatia tamko la serikali lililotolewa kwa nyakati tofauti na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati wa Mkutano wa wadau wa kilimo cha pamba kutoka Mikoa kumi hapa nchini kilichofanyika mwezi Mei mwaka huu Jijini humo na lile la Rais Dkt. Jakaya Kikwete alilolitoa wakati wa majumuisho ya kuhitimisha ziara yake ya siku tano Mkoani Mwanza hivi karibuni.
Mwenyekiti Festus Limbu (katikati).
Mwenyekiti wa Baraza la Wakurugenzi Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) Dr.Festus Limbu (Mb) alisema kuwa uamuzi huu umepelekea Bodi hiyo kutoa tamko la Taasisi hiyo Muhimu nchini inayosimamia zao la Pamba hapa nchini kutangaza kuwa kuanzia mwezi Novemba mwaka huu utekelezaji wa Kilimo cha Mkataba utaanza kwa Mikoa kumi ya Kanda ya Magharibi inayojishughulisha na kilimo cha zao.
“Tumezamilia kurejesha ubora wa Pamba Nyeupe zamani ikijulikana ‘Dhahabu Nyeupe’ kwa kuhakikisha msimu huu wa Kilimo wa mwaka 2013/2014 unaoanza mwezi Novemba mwaka huu kila Mwekezaji na mnunuzi wa pamba kuanza kuwekeza kwenye Kilimo cha Mkataba ambacho kimsingi ndiyo kitakuwa suruhisho la Mkulima kunufaika na Mwekezaji huyo hali itakayosaidia pamba kurejea kuwa na thamani na ubora” alisema Dr.Limbu.
Mwanyekiti huyo  alisema kuwa utekelezaji wa Mkataba huo utakuwa ni kati ya Wanunuzi, Wamiliki wa viwanda vya pamba na wakulima ambapo watatakiwa kupeleka kwenye maeneo ya wakulima vijijini Pembejeo za kilimo ikiwa ni Mbegu za Quton, Mbolea na Madawa ya kuulia wadudu na kufunga Mkataba na wakulima huku viongozi wa serikali za vijiji na vyama vya msingi wakiwa mashahidi.
Dr Limbu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Magu Mkoani Mwanza, alisema  tamko la serikali juu ya uamuzi wake wa utekelezaji wa kilimo cha Mkataba katika tasnia ya Pamba pamoja na kuwa na tija ndogo katika uzarishaji ambapo uzarishaji kwa umekuwa wa Hekali moja kutoa kilo 300 ikilinganishwa na lengo la kuzalisha kilo 1,500 kwa Hekali moja ifikapo mwaka 2015 kote nchini.
“Tunazo changamoto nyingi ikiwemo ya uhaba wa viwanda vya kuongeza thamani, matumizi madogo ya pembejeo, kutolewa kwa pembejeo muda ukiwa umepita, kilimo kutegemea mvua za msimu na wanasiasa kutumia mwanya wa kujipenyeza na kuwachezea wakulima jambo ambalo limeonekana kabisa kusababisha ubora hafifu unaosababisha pamba kuuzwe kwa bei punguzo na kumnyonya mkulima” alisema na kuongeza kuwa
Tasnia ya Pamba ni muhimu katika uchangiaji wa pato la taifa na tegemeo la asilimia 40 ya Watanzania, lakini kilimo cha zao hilo kimekuwa kikikabiliwa na matatizo mengi na changamoto mbalimbali hali inayoonekana kudidimia kwa zao hilo kila msimu hivyo kupitishwa kwa mswada wa sheria ya kuanzishwa kilimo cha umwagiliaji kutakuwa mkombozi kwa wakulima. 
“Sekta hiyo binafsi itabidi iwekeze katika kuwapatia wakulima pembejeo na huduma zingine, badala ya kusubiri kwenda kununua pamba kwa wakulima mwishoni mwa msimu, kwa sababu mfumo wa sasa wa mnunuzi kupewa jukumu la kukusanya fedha kutoka kwa mkulima na kuziwasilisha CDTF umeonekana kuwa na matatizo makubwa” alisema Dr. Limbu

Aliitaja Mikoa ya Kanda hiyo itakayo tekeleza kilimo cha mkataba kuwa ni Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Mara, Kagera, Tabora, Geita, Singida, Rukwa na Kigoma na kwamba wadau wote walio na nia ya kununua pamba msimu ujao, waanze kusambaza mapema mbegu na pembejeo (Quton) kwa wakulima ili mwakani wanunue pamba kutoka kwao na si kuvamia kununua kiholela kama ilivyo sasa.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa Kampuni ya ununuzi wa pamba na kiwanda kitakachoshindwa kupeleka pembejeo za kilimo kwa wakulima katika utekelezaji wa Kilimo cha Mkataba kuanzaia mwaka huu wa msimu wa kilimo mwezi Novemba, mwakani waklati wa kuanza msimu wa ununuzi wa pamba haitapatiwa Leseni na Bodi ya Pamba na halitaruhusiwa kuvamia kiholela kununua Mikoa yote.

“Leseni za ununuzi wa pamba zitatolewa kwa kuzingatia kigezo cha uwekezaji wa kila mdau katika eneo husika na si vinginevyo na hakutakuwa na ujanja ujanja kwenye kufunga mkataba na wakulima wa zao hilo ieleweke na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya Kampuni husika na wakulima hawataruhusiwa kuuza pamba yao kwa mtu ambaye hakuwapa pembejeo. 

Aidha Dr Limbu alisema kuwa katika kuhakikisha utekelezaji huo unafanikiwa Ofisi za wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zitasimamia kwa karibu utaratibu huo mpya wa kilimo cha mkataba ili malengo ya kuondokana na matatizo yanayoathiri kilimo hicho yafikwe huku wachafuzi wa pamba wakati wa msimu wa kuuza pamba wakiwekewa mwarobaini wa kuwadhibiti.
CHANZO: GSENGO BLOG

Thursday, 18 July 2013

Kampuni ya Airtel yazima laini za simu zisizosajiliwa 200,000 ili kuongeza usalama Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Bi Beatrice Singano
Airtel yazima laini za simu zisizosajiliwa 200,000 ili kuongeza usalama Dar es Salaam, Tanzania 18 Julai 2013, Airtel Tanzania imetangaza itetimiza tamko la serikali la kuzima laini za simu ambazo hazijasajiliwa ikiwa ni utekelezaji wa sheria ya posta na mawasiliano ya kielektroniki ya mwaka 2010 na  muda wa hitimisho wa kusajili namba uliowekwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)  wa tarehe 10 Julai 2013
 Usajili wa namba ni mchakato wa kuhakiki na kuweka kumbukumbu za mtumiaji wa namba ya simu unaowekwa na mtoa huduma za mawasiliano ya simu, maelezo ya usajili ni pamoja na namba ya simu, tarehe ya kuzaliwa, jinsia, sanduku la posta, namba nyingine ya simu kama ipo, kitambulisho na namba ya kitambulisho kilichowakilishwa

Akiongea kwa niaba ya Airtel , Mkurugenzi wa Mawasiliano na Usimamizi wa Sheria Beatrice Singano alisema" wateja wetu wote walijulishwa mapema kusajili simu zao na tumetoa muda wa kutosha kwa zoezi hili la usajili kufanyika ili kuepuka kufungiwa simu zao.  Tumetimiza sheria kama inavyosema ya EPOCA na kufunga simu zote ambazo hazijasajiliwa
kuanzia usiku wa tarehe 10 julai kama mamlaka ya mawasiliano ilivyowatangazia mwezi wa April mwaka huu, kwa sasa jumla ya wateja wetu 200,000 tumewafungia mawasiliano kwa kutotimiza tamko hili la kusajili namba zao za simu za Airtel

Tunaamini kwa kufungia simu hizi kuna wateja watabaki bila mawasiliano hivyo tunachukua nafasi hii kuwaomba  wateja ambao hawajasajili simu zao kufanya hivyo  katika vituo vyetu vya huduma ikiwemo,  maduka yetu ya Airtel, wauzaji wa bidhaa zetu wa rejareja na  mawakala wetu wote nchi nzima. Pia kwa wateja wanaonunua namba mpya kuanzia sasa wasajili namba zao ili waweze kuzitumia. Pamoja na hilo pia tunawashauri wateja waliosajiri kuhakiki usajili wao kwa kupiga*106#. Tunaamini zoezi la
usajili litasaidia kudumisha Amani na usalama wa watanzania na zaidi ya yote kukuza sekta ya mawasiliano.

Usajili wa namba za simu umekuwa ukiendelea kwa miaka michache katika ukanda wa jumuiya ya Afrika mshariki (EAC)  ikiwa na lengo la kudhibiti matukio yanayofanyika kwa kutumia namba zisizosajiliwa ikiwemo, wizi kwa njia ya mtandao, utekaji, ujumbe wa matusi, ugaidi na mengine mengi

Kenya na Tanzania imepiga hatua na kufikia zoezi la kuzima simu nchi nyingine za jumuiya ziko katika atua ya awali za utekelezaji, Uganda iko katika hatua ya utekelezaji wa usajili wa namba za simu.

Duniani kote mtumiaji wa simu anatakiwa kusajili simu kadi yake mpaka pale itimisho linapotokea . na mteja yoyote anayeshindwa kusajili simu yake mpaka muda wa hitimisho simu yake itafungiwa na mteja atapoteza namba yake, hivi karibuni usajili wa namba umeendelea katika nchi za Ghana, Sierra Leone Nigeria, Zimbabwe, South Africa, Kenya, Singapore,
Malaysia, Geneva, India, Egypt na nchi nyingine 

Singano amewakumbusha mawakala na wasambazaji wa Airtel kutimiza agizo hili na kuhakikisha kuwa simu kadi yoyote inayouzwa au kupewa mteja iwe imesajiliwa kabla ya matumizi, ni kosa la jinai kutumia simu kadi isiyosajiliwa

"Mchakato huu ni wa lazima chini ya sheria ya posta na mawasiliano ya kielektronikia (EPOCA) ya 2010 inayotoa jukumu la muuzaji au mtumiaji wa simu kusajili namba zao kabla ya kuitumia. Na usajili wa namba katika vituo vyetu vya wasambazaji mawakala nchini nzima ni bure aliongeza Singano

chini ya kifungu cha 130 cha sheria ya posta na mawasiliano ya kielektronikia (EPOCA) ya 2010  ni marufuku kwa mtu yeyote kuuza namba ya simu kwa mtu yeyote bila kuweka kumbukumbu za mtumiaji wa namba hiyo.

Thursday, 11 July 2013

MWANAMKE ALIYETUPA MTOTO CHOONI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 5 JELA MKOANI MBEYA


Rukia Haruna (31) akitolewa nje ya mahakama na askari  kwenda gerezani kutumikia kifungo cha miaka mitano.…
Rukia Haruna (31) akitolewa nje ya mahakama na askari  kwenda gerezani kutumikia kifungo cha miaka mitano.
Pichani juu ni taswira za wananchi wa eneo la Manga A jijini Mbeya wakati wakijaribu kuokoa maisha ya kichanga  kilichotupwa chooni na Rukia Haruna Juni 14 mwaka huu.
Picha iliyozibwa ni ya kichanga kilichotupwa baada ya kutolewa chooni.

Mwanamke Rukia Haruna (31), mkazi wa Manga A Jijini Mbeya, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kutupa mtoto wake chooni.
Tukio hilo lilitokea Juni 14, mwaka huu katika eneo hilo baada ya watoto waliokuwa wakicheza kugundua kuwepo kwa mtoto katika choo cha shimo.
Mtuhumiwa baada ya kukamatwa amekiri kutenda kosa hilo na kwamba alifanya hivyo baada ya mzazi mwenzie kumkataa.
Ameongeza kuwa alilazimika kutupa kichanga hicho katika choo cha jirani kwa sababu ni cha shimo tofauti na chao ambacho asingeweza kutupa mtoto huyo.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa, mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Zabibu Mpangula, amemhukumu mtuhumiwa kifungo cha miaka mitano baada ya kosa hilo ambalo ni kinyume cha kifungu  218 kifungu kidogo cha 35 sura ya 16 ya mwaka 2002.
HABARI NA MBEYA YETU BLOG

RAIS JK AFUNGA KONGAMANO LA KITAIFA KUJADILI AMANI

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya kufunga Kongamano la Kitaifa Kujadili Amani ya Taifa lililofanyika katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salam  Jana jioni.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya kufunga Kongamano la Kitaifa Kujadili Amani ya Taifa lililofanyika katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam jana jioni.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Centre for Democracy (TCD) ambaye pia ni kiongozi wa chama cha NCCR Mageuzi Mhe. James Mbatia akimkabidhi Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete maazimio ya Kongamano la Kitaifa kujadili Amani ya Taifa lililofanyika katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam na kufungwa  Jana jioni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wa vyama vya siasa vilivyoshiriki katika Kongamano  la kitaifa Kujadili Amani ya Taifa lililofanyika katika Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.Kushoto ni kiongozi wa Chama cha NCCR Mageuzi Mhe.James Mbatia (MB), Mwenyekiti wa TLP Mhe.Augustine Lyatonga Mrema(watatu kushoto) na kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha UDP Mhe.John Momose Cheyo
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(aliyekaa katikati) Akiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa na washiriki wa Kongamano la Kitaifa Kujadili Amani ya Taifa lililofanyika katika Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.
                                       (PICHA NA FREDDY MARO)

Tuesday, 23 April 2013

BREAKING NEWSSS MWENYEKITI WA UMOJA WA SACCOS TAIFA NA PIA NI MFANYAKAZI WA TAZARA MBEYA AMBROSE LUCAS SHAYO APIGWA ATESWA NA KUCHOMWA MOTO.

HAPA NDIPO ALIPOTESWA NA KUUWAWA AMBROSE SHAYO
HAPA NDIPO ALIPOCHOMWA MOTO NA WATU WASIOJULIKANA

HILI NDILO ENEO GARI YAKE ILIPINDUKA NA WAUWAJI WALIPOPATA NAFASI YA KUMUUA AMBROSE
HAPA NDIPO GARI YA AMBROSE ILIPOGONGA NA KUPINDUKA WAKATI ANAKIMBIZWA NA WAUWAJI HAO

HABARI KAMILI YA TUKIO HILI TUTAZIDI KUWAJULISHA KWANI  POLISI WANAENDELEA NA KAZI YAO. NA MBEYA YETU BLOG.

Monday, 22 April 2013

MWONEKANO MPYA WA GAZETI LA MWANANCHI MBEYA, PATA PICHA HALISI ZA TUKIO ZIMA.


Mkurugenzi Mtendaji wa MCL Tido Mhando akizungumza na wadau mbali mbali jijini Mbeya katika sherehe ya kutangaza mwonekano mpya wa gazeti la Mwananchi
Mkuu wa wilaya Mbeya akiwapongeza wafanyakazi wa MCL kwa kuwahabarisha wananchi kote nchini 
Wadau na wafanyakazi wa Mwananchi wakiangalia makala fupi toka lilivyo anza gazeti la mwananchi mpaka sasa kwenye mwonekano mpya
Baadhi ya waandishi wa MCL
Wadau mbali mbali wakisherehekea mwonekano mpya wa gazeti la mwananchi